Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amemuagiza OCD kukamata mara Moja mkurugenzi wa Kampuni ya Plancon Ltd Kwa kushindwa kutekeleza ujenzi wa mradi bwawa la maji ya kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Matekwe
Moyo alisema kuwa kampuni hiyo imeshindwa kukamilisha mradi wenye thamani ya Shilingi 405,757,160.00 ambao ulitakiwa kukamilika April 2022 lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika
Alisema kuwa Bwawa hilo linauwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo 102,000 kwa wakati mmoja kulingana na hali ya mvua huku ikitarajiwa bwawa hilo litahudumia ng’ombe 9,992,mbuzi 2,711 na kondoo 489.
Hivyo mkuu wa wilaya ya amesema akamatwe mara Moja huyo mkurugenzi popote pale alipo akamatwe apelekwe Nachingwea kukumilisha mradi wa Bwawa katika Kijiji cha Matekwe.
0 Comments