Header Ads Widget

BILIONI 234.1 KUKARABATI SKIMU ZA UMWAGILIAJI.


Na Hamida Ramadhan-Matukio Daima APP, Dodoma.

HADI kufikia Juni 2023,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imesaini mikataba 48 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 234.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa skimu na mabwawa ya umwagiliaji.


Hayo yamesemwa leo Jijini hapa na Mkurungezi Mkuu wa tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa Wakati akielezea utekelezaji wa majukumu yake na uelekeo kwa Mwaka wa fedha 2023/24


Pia wamesaini Mikataba 22 yenye thamani ya shilingi Bilioni 25 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Mikataba mitatu (3) yenye thamani ya Shilingi Bilioni 23.9 kwa ajili ya ununuzi wa magari na mitambo

Aidha amesema Tume imenunua magari 53 kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya umwagiliaji.


Tume pia imefanikiwa kupata fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa PFoR ambapo utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2023/2024; Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 70 kwa miaka mitano.


Mkurungezi huyo amesema, Tume imefanikiwa kupata fedha kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kupitia mradi wa “Irrigation Development Advisory”.Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.


Amesema Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, mwelekeo wa Tume ni kuendelea kutekeleza miradi itakayoongeza eneo la umwagiliaji lenye ukubwa hekta 256,185.46 ili kufikia hekta milioni 1,200,000 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2020),


Ameeleza awamu ya Tatu ya Mpango Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III; 2021/2022-2025/2026) na Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) na kufikia hekta milioni 8.5 ifikapo 2030 (Agenda 10/30).


" Ili kufikia malengo hayo Tume imepanga kutekeleza jumla ya miradi 822, ambapo miradi 114 ni ya ujenzi wa mabwawa na 103 ni ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji," amesema Mkurungezi huyo.


Hata hivyo Amesema katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 Amesema Kipaumbele chao ni kukamilisha ujenzi wa skimu mpya 25 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI