Header Ads Widget

ASKOFU WILBARD AWAWAKIA WATANZANIA KUHUSU MKATABA WA BANDARI (DP WORLD)

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


ASKOFU Wilbard Ringia wa Kanisa la Mizaituni miwili,Pentecoste Assemblies(MMPA) amewataka Watanzania kuwa watulivu na wenye kuheshimu mamlaka ili mambo mengine yaendelee kutokana na kuwepo maneno mengi ya kubeza Mkataba wa uwekezaji wa Bandari (DPWORLD)


Askofu Ringia ameyasema hayo leo Julai 16,2023 Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na uwekezaji huo ambapo amesema maneno mengi yanayobeza hayautukuzi utukufu wa Mungu.


Amesema Mamlaka zote ulimwenguni huwekwa na Mungu hivyo watanzania hawapaswi kuwa na hofu na serikali iliyopo madarakani kwani kila jambo linalotokea limepangwa na Mungu.


“Tuiachie Serikali ifanye maamuzi na hatma ya maendeleo yetu kwa sababu inao wataalamu wengi ,nataka niwaambie watanzania kuwa Serikali huwa haikurupuki bali huanza kufanya upembuzi wa mambo kupitia wataalamu wake kabla ya kutoa suluhu,msiwe na wasiwasi,”amesema na kuongeza;


Amesema Kila mwanadamu ameumbwa na mungu,hata kuwepo madarakani kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan pia ni mipango ya Mungu.


 "Hivyo Basi hatuna sababu ya kumlalamikia kwani yote anayoyafanya yanatokana na Mwenyezi Mungu kwa kuwa tunaamini Mungu humtengeneza mtu kuwa Kiongozi tangu anapokuwa tumboni mwa mamaye," Amesema Askofu huyo


Aidha amesisitiza kuwa Mamlaka ya Mungu yanaanzia duniani kupitia viongozi wakuu wanchi hivyo watanzania hawapana haja ya kuwa na shaka na maamuzi yoyote yanayotolewa na viongozi hao.


"Haisaidii kuleta maneno maneno uwekezaji ni jambo muhimu mno kila mtu anajua, Ningeshauri tuheshimu mamlaka ya nchi na kufuata maelekezo ya viongozi wa dini ili kuwa na maarifa zaidi,najua yote haya yanatokea kwa kuwa watu wengi hawana maarifa , watu wanapotea kwa sababu hawajui maandiko,hebu kila mmoja asimame kwenye nafasi yake ili tuungane kuijenga nchi yetu,”amesema


 Na kuongeza Kusema"Sio adabu wala heshima kumdharau Rais tumpe nafasi ashughulikie uchumi wetu, Mungu ataki fujo wala kudharauli,”amesisitiza


Askofu huyo pia ametumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania kukataa kuishi kwa kusikiliza hadidhi za uongo zinazokwamisha maendeleo na badala yake  wafuate muongozo wa Serikali inavyotaka.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI