Header Ads Widget

WANASIASA WAONYWA KUACHA KUWAPOTOSHA WANANCHI MCHAKATO WA BANDARI

 


Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga.


KATIBU wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (Jwt) Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuwapotosha wananchi juu mchakato wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo na kuimarisha utekelezaji wa bandari za Bahari na Maziwa Nchini Tanzania.


Kauli hiyo ameitona jana wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wanaoishambulia Serikali ya Tanzania juu ya ushirikiano na Serikali ya Emirati ya Dubai (DP WORLD) katika swala la uwendeshaji wa Bandari ya Dar esa Salaam kwa kile wanachodai bandari hiyo  imeuzwa.


Masoud ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Maalum ya Waziri Mkuu ambayo iliundwa baada ya kutokea mgomo wa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo alisema wanasiasa hao wamekuwa vinara wa kuzungumzia siasa zaidi badala ya kuzungumzia kasoro ili Serikali iweze kuzirekebisha kwa maslahi ya Taifa.


"Kumekuwepo na mijadala mingi ya kisiasa na baadhi yao ndio wamefanya kuwa agenda zao kama wao sio Watanzania lakini watambue kuwa Serikali yetu iko makini na haijakurupuka katika mchakato huo"Alisema Masoud. 


Aidha alisema mkataba uliopo sasa sio wa utekelezaji bali ni mkataba wa makubaliano ya awali kwa pande zote mbili na ndio unaolinda majadiliano baina Serikali ya Tanzanian na ile ya  Emirati ya Dubai kupitia Kampuni ya Dubai Ports World (DP WORLD)


Alisema wanasiasa kukosa sera na hoja za msingi ndani ya vyama vyao kumepelekea kukosoa mambo ya msingi yanayofanywa na kutekelezwa na Serikali kwa maslahi ya Watanzania wote bila ya kuangalia itikadi ya vyama vyao. 


Hata hivyo Masoud ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu wake wa kutaka kudhibiti mianya ya ubadhirifu kupitia mchakato huo.


Alisema si rahisi kuweza kubaini vita iliyopo juu ya utekelezaji wa mchakato huo ambao unawagusa vigogo wengi ambao kwa namna moja au nyingine wananufaika na bandari hiyo ya Dar esa Salaam. 


"Nimpongeze Rais wetu kwa hatua anayoifanya ya kukata mcheni ya ubadhirifu katika bandari yetu lakini mchakato utakapokamilika tutakuwa miongoni mwa Nchi zenye bandari bora Duniani na ya kisasa zaidi"Alisema .


Amemuomba Rais na Serikali yake kuwapuuza wakosoaji na badala yake atumie mamlaka zake kuharakisha mchakato huo ambao ndio utakuwa muarubaini kwa kukuza pato pato la Taifa kupitia bandari hiyo na kudhibiti mianya ya ubadhirifu bandarini hapo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI