Header Ads Widget

AFISA MAUZO MBARONI KWA KUGHUSHI VYETI VYA UDEREVA

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Afisa mauzo wa kampuni ya Chloride Exide John Msemo wenye umri wa miaka 45 na wengine nne wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Mwanza Kwa kujihusisha na makosa ya kughushi vyeti na leseni za udereva vinavyotolewa na chuo Cha veta.


Akitoa faarifa hiyo Kwa waandishi wa Habari kamanda wa polisi Mkoani hapa Wilbroad Mtafungwa Amesema kuwa watuhumiwa wote walikamatwa Kwa nyakati tofauti tofauti baada ya jeshi Hilo kupitia kikosi Cha Usalama barabarani kuanza ukaguzi wa vyeti na leseni Kwa madereva wa magari.


Mtafungwa amewataja watuhumiwa mwengine ni pamoja Esau Yakobo mwenye umri 26 Mkazi wa mecco kaskazini, Sixmond George miaka 48 mkufunzi wa chuo Cha udereva Nyanza na Mkazi wa igoma, Samwel Bose miaka 47 mwalimu wa chuo Cha udereva chanila na Mkazi wa ibanda juu.


Ameeleza kuwa watuhumiwa walikamatwa wakiwa na vyeti vyenye majina, namba na vivuli vya leseni za udereva pamoja na picha mbalimbali za passport size na barua za polisi ambazo zimeghushiwa Saini ya Mkuu wa kikosi Cha Usalama barabarani Mkaoni hapa.


Aidha Kwa upande mwingine ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa na barua ya kughushi iliyohusu uhakiki wa leseni kutoka jeshi la polisi ambazo wamekuwa wakitumia kujinufaisha Kwa kuwadanganya wananchi Kwa kuwatengenezea vyeti batili.


"Jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata mtandao wa waalifu hao na vifaa walivyokuwa wakitumia kughushi nyaraka hizo ikiwemo printer moja aina Epson, computer aina HP na Flash mbili" Alisema Mtafungwa.


Aidha Mtafungwa amesema kuwa watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani bada ya upelelezi kukamilika na kuwata madereva wote pindi wanapoliza kusoma kuchukua vyeti na kuachana na tabia ya kughushi vyeti.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI