Na Gift Mongi - Dodoma.
Katika kuhakikisha wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini wanapatiwa huduma stahiki hususan zile za kiafya jitihada mbali mbali zinaendelea kufanyika kama ambavyo ni dira ya serikali ya awamu ya sita.
Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na maswali ya msingi ambayo serikali imekuwa ikihojiwa bungeni kwa mara kadhaa kupitia mbunge wa jimbo hilo Prof Patrick Ndakidemi.
Mfano hii juzi bungeni mbunge huyo aliuliza swali la nyongeza bungeni lenye kuleta matumaini kwa wahitaji wa viungo bandia kama ifuatavyo;
Je? Serikali ina mpango gani wa kusaidia wagonjwa wanaohitaji viungo bandia kama vile miguu bandia kwani gharama zake ziko juu sana kwa wananchi wa kawaida.
Hata hivyo majibu kutoka serikalini kupitia naibu waziri wa afya Dkt Godwin Mollel yameonyesha faraja kwa wahitaji hao wa viungo bandia na kuwa serikali inaweka mazingira rafiki yasiyokuwa na urasimu katika kupata huduma hiyo.
Gadnael Charles mkazi wa Kibaigwa anasema huduma za matibabu zimekuwa ghali na kuwa wananchi walio wengi wamekuwa wakishindwa kumudu gharama hizo.
'Tunashukuru hata kusikia viongozi wanapokumbuka haya mambo maana gharama zimekuwa kubwa sana ikilinganishwa na hali ya kipato chenyewe'anasema
Kwa upande wake Nginaeli Tillya mkazi wa Kirima wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro ambaye ni mlemavu wa mguu amesema jitihada hizo zinazoendelea zinaleta faraja kwa makundi hayo kwani walionekana kama kusahaulika.
'Kiukweli mbunge wetu Prof Ndakidemi amekuwa na maono ya kipekee katika kutukumbuka na sisi nadhani sasa ni mwanga mpya kwetu sisi wenye ulemavu maana kama tulitengwa vile'amesema
Mwisho.
0 Comments