Na Mwandishi wetu, Mtwara
Mmiliki wa Kampuni ya Shebby mix ya Mkoani Mtwara Shabani Mmolole amewahamasisha wahitimu wa vyuo vikuu kujiajiri wenyewe na kuacha kufikiria ajira na kuwataka kuchangamkia fursa kubwa zilizopo nchini ili kujiiinua kiuchumi.
Akizungumza katika Maafali ya seneti ya UVCCM yaliyojumuisha vilivyopo Mkoa wa Mtwara alisema kuwa utayari unaweza kutengenezwa ili kuzichangamkiwa fursa kwa mazingira tofauti tofauti ambazo zipo ndani na nje ya nchi yetu.
alisema kuwa zipo fursa nyingi nchini vijana wakijiandaa na wakajitoa wanaweza kufika zaidi kwakuwa seriklai imetengennza njia nyingi za kuwezesha vijana kuona na kufanya jambo kwaajili ya nchi yao”
“Rais Samia Suluhu anafanyakazi kubwa lazima tutambue katika maisha ya viongozi lazima kuwe na daraja kila daraja likitimiza wajibu wake kazi itafanyika vizuri ambapo Mchakato wa maendeleo inahitajika msaada katika utekelezaji.
“Serikali nafanya mambo makubwa yenye fedha nyingi na kuwajali watanzania niwaombeni nendeni mkaisaidie serikali mkifika nendeni kwenye seirklai za mitaa fedha zinazoletwa na maendeleo yaliyopo yanafanana Sisi wasomi ndani ya chama hakuna aisie fata taratibu kanuni na sheria”
Nae Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mtwara Abuu Athuman Yusuph alisema kuea wahitimu wa vyuo vikuu mkoa wa Mtwara wawe na utayari wa kuchangamkia fursa mbalimbali zinaozoweza kuwawezesha kujiajili wenyewe.
Alisemakuwa ni vema kujiongeza na kuona changamto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi hasa katika wakati huu ambao nchi yetu ina uwekezaji mkubwa sana ili kumuwezesha kijana kujiajiri.
“Unafurahi kwakuwa serikali imetoa ada ya lessen ya kuanzisha biashara hiyo ni fursa kubwa ndni ya mwaka kijana anauweza kufanya vizuri zaiid ni namna serikali imeweza kufanya ili kumshawishi kijana kujiongeza”
0 Comments