NA HADIJA OMARY, LINDI
Wananchi na wadau wa Maji mkoani Lindi, wameyapinga mapendekezo mapya ya bei za Maji kwa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa mazingira Mjini Lindi LUWASA hii ni baada ya Mamlaka hiyo kupendekeza bei mpya na za juu kwa kigezo cha kushindwa kutoa huduma yenye viwango kwasababu za ukata wa fedha.
Wakizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na mamlaka hiyo ya maji, chenye lengo la kutambulisha bei mpya kwa wateja wake baadhi ya watumiaji wa huduma hiyo akiwemo Abeid Bakari wameishauri LUWASA kutafakari upya na kupanga bei wanayoweza kuimudu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye kikao hiko na kaimu mkurugenzi wa Luwasa Mkoa wa Lindi bei ya awali kupanda ni kutoka shilingi 1600 hadi 4690 kwa uniti 0-5 majumbani, ambapo alieleza kuwa upandaji huo ni kutokana na mamlaka kukumbwa na ukata wa fedha kulikopelekea kuwa na madeni ya umeme pamoja na kuhitaji kufanya maboresho ya miundombinu
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, aliwasihi LUWASA kupendekeza bei nafuu ambayo wananchi wangeimudu huku akikiri kufahamu hali yao ya uchumi inayopitia Mamlaka hiyo kwa sasa.
Kwa upande wake Mjumbe ushauri MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA Conrad Milinga wameishauri LUWASA kujadili upya bei hizo na kuziwasilisha kwa mamlaka za juu ili kutambua kwa umakini namna ya kuwasaidia wananchi na wanufaika wote wa huduma hiyo ya maji.
0 Comments