Header Ads Widget

JAMII YAASWA KUZINGATIA MAADILI

 

Na Pamela Mollel,Arusha 

Jamii imeaswa kuzingatia maadili na kuacha vitendo viovu na kufanya yale yanayompendeza Mungu ikiwemo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu katika nafasi tunazopewa ili nchi iweze kuwa na maendeleo na kupiga hatua kiuchumi.


Hayo yameelezwa na  Baba Askofu Dkt. Solomoni Jacob  Massangwa ambae pia ni Mkuu wa Dayosisi ya kaskazini kati  kanisa la kilutheri Tanzania  katika ibada ya kumstaafisha  parishworker wa jimbo la Arusha Mashariki  Bi. Rebeca Christopher Mungure ambae amekuwa kwenye utumishi takribani miaka 40.


Askofu Dkt. Solomoni Masangwa alisema kuwa jamii kwa ujumla inapaswa kuiga mfano mzuri kutoka kwa Parishworker huyo aliyejitoa kumtumikia Mungu tendo ambalo limempendeza Mungu na wanadamu


"Viongozi na watumishi katika Taifa letu la Tanzania ni vizuri kuiga mfano wa Bi.Rebeca kwa kufanya kazi kwa bidii,maarifa na uaminifu pamoja na uvumilivu mkubwa na mwisho wao utakuwa baraka kwao na kwa Taifa letu"alisema Baba Askofu 


Kwa upande wake Bi. Rebeca baada ya kustaafu kwa heshima akatoa shukrani zake kwa Dayosisi na Kanisa huku akipanda mti kama alama ya  kumbukumbu katika usharika wa Kimandolu


"Namshkuru Mungu sanaaa kwa tukio kubwa  la leo la kustaafu kwangu kwa heshima nawashukuru sana Dayosisi na kanisa wakiongozwa na Mkuu wa jimbo letu la Arusha Mashariki Mch.Daniel Mahawe kwa kuwa mstari wa mbele kwa jambo hili"alisema Bi.Rebeca


Aidha aliwashukuru wote waliojitoa kwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha na gari alilozawadiwa na idara ya wanawake 


Naye Mwenyekiti idara ya wanawake jimbo la Arusha mashariki Bi. Nembrisi Samwel akaeleza utumishi wa mfano aliokuwa nao bi. Rebeka hivyo wakina mama  wamemwaga   kwa kumzawadia gari yenye thamani ya sh. Milioni 14 na kueleza kuwa huu uwe mfano kwa jamii katika utumishi wa uaminifu









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI