NA THABIT MADAI - ZANZIBAR
MAMLAKA ya Masoko na Mitaji (CMSA) kwa kushirikiana na Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na Vya Kati Zanzibar (SMIDA) wameendesha semina ya kuwajengea uwezo na uwelewa wadau ambao ni wafanyabiashara, wajasirimali na Wakufunzi kuhusu mpango wa kuwezesha kupatikana fedha kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo za kati.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Utalii Maruhubi Mjini Unguja na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 80 Wajasiriamali ,wafanyabiashara pamoja na Wakufunzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo, Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charse Shilima amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na uelewa wadau wakiwemo wanyabiashara ndogo ndogo na kati pamoja na wajasiriamali kuhusu mitaji halaiki.
"Tumeendesha Semina hii ili kuwajengea uwezo na uwelewa wa kutambua fursa za kuweza kupata mitaji na kukuza biashara zao na kujikomboa na umasikini,"amesema.
Aidha amewataka Wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali kujianda kulitumia jukwa la Mitaji halaiki kupata Mitaji kwa lengo la kukuza biashara zao pamoja na kujikomboa na umasikini unaochangiwa na ukosefu wa ajira nchini.
Amefahamisha kuwa jukwa hilo hilo litakuwa na nafasi ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali kuomba mtaji kwa kuuza wazo la biashara pamoja na hisa.
Aidha ameeleza kuwa jukwaa hilo linatazamiwa na Serikali kuwa mkombozi wa Wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na Wafanyabiashara wa Kati.
"Jukwaa hili linawaunganisha pamoja Wafanyabiashara, Wajasiriamali wadogo na wakati ambapo wanaweza kupata mitaji kwa kuuza wazo la biashara," ameeleza.
Mapema Mkurugezi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo Vidogo na Vya Kati Zanzibar Sudu Saidi Ali anasema Ujio wa Jukwaa la Mitaji Hailiki ni mkombozi wa Bidhaa na Biashara zisizopata Mikopo Mitaji kutoka kwa Wafadhili.
Nao Washiriki wa Semina hiyo Aisha Said Omari pamoja na Hafidhi Mohammed Salim wamesema kuwa, Semina hiyo ni muhimu kwao kutokana na manufaa ambayo wanayoyapata ya kujua namna ya kupata mitaji.
"Katika Semina kama hizi zinatusaidia katika kujua namna ya kukuza biashara zetu tunaozifanya takribani kila siku kwa kupatiwa mitaji halaiki," wamesema.
0 Comments