Header Ads Widget

KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AWATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI.








NA HADIJA OMARY,Matukio Daima App 

Katibu mkuu wizara ya maji mhandisi Nadhifa  Kemikimba amewataka wakandarasi wawili M/STC CONSTRUCTION COMPANY LIMITED NA M/S. EMIRATES BUILDERS’ CONSTRUCTION. LIMITED wanaotekeleza mrasi wa maji katika Wilaya za Lindi, Ruangwa na Nachingwea Mkoani Lindi  wenyethamani ya shighuli Bilion 119 kukamilisha mradi huo kwa wakati.


Kemikimba amebainisha hayo alipofanya zihara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo ambapo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ni kuwafanya wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.

Alisema wizara yake itaendelea kufanya ufuatiliaji katika mradi huo mpaka hatua ya mwisho ili kuona mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa

" tunamshukuru Rais wetu Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutuona wizara ya maji na kutupatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali hapa nchini hii yote ni kutaka kuona akina mama hawa wanatuliwa ndoo kichwani" alisema mhadisi Kemikimba.

Kwa upande wake Meneja wa Ruasa Mkoa wa Lindi mhandisi Muhibu Rubasa amesema mradi huo utakapikamililika unatarajia kuwanufaisha wananchi wapatao  Laki moja na Elfu ishirini na tqtu elf  mia sita na hamsini na saba kutoka katika vijiji 56 vitakavyonufaika na mradi huo 


Hata hivyo alisema kuwa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia tano ya utekelezaji na kwamba kazi zinazoendelea hivi sasa ni kusafisha maeneo ya utekelezaji wa mradi huo

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Nandagala Halmashauri ya Ruangwa wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Adrew Chikongwe wamesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya upatikanaji wa maji safi na salama  waliyokuwa nayo hapo awali


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI