Header Ads Widget

SHEIKH HASSAN: WANANDOA MUWE NA SUBIRA SUALA LA KUPATA MTOTO.

 


Na chausiku Said, Matukio Daima App Mwanza 

Chanzo Cha kutopata Mtoto ndani ya familia imekuwa ni Changamoto inayopelekea familia nyingi kuwa na migogoro ya mara Kwa mara na kusababisha wanandoa kutengana.


Hayo ameyabainisha na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke katika swala ya Eid Al- Adhaa ( Eid ya kuchinja) iliyoswaliwa katika viwanja vya Nyamagana Wilaya Nyamagana Mkoani hapa na kueleza wanandoa kuwa na subira katika swala hilo hakuna mtu  anayependa kukosa Mtoto.



Kabeke amewataka waumini wa kiislamu kuendelea kuwa wavumilivu katika ndoa hususani katika kipindi kigumu wanachopitia Cha kukosa Mtoto na kuacha na kutumia njia zisizo salama.


"Wanandoa wanapaswa kuvumiliana , ndoa nyingi zinateteleka Kwa sababu ya kukosa Mtoto na kusababisha mateso kuishi Kwa mateso Kwa mawifi, wakwe na wakati mwingine wanaume wenyewe kusababisha mateso Hayo" Alieleza Kabeke.


Alifafanua kuwa swala la kupata Mtoto linatoka Kwa Mwenyezi Mungu ndio anapanga kuhusu swala hilo na kumpa mtu mtoto amtakaye na, Mungu huyo huyo  ndio anauwezo wa  kumnyima Mtoto mtu.


"Emu tukumbuke kisa Cha Ibrahim Sala waliopata Mtoto umri ukiwa umeenda mmoja akiwa na umri wa miaka 90 na mwingine 86 Alisema Kabeke.


Aidha Kwa upande mwingi amewataka waislamu wote kuhakikisha wanakuwa na malezi Bora Kwa watoto wao ili kuepukana na Mmomonyoko wa maadili uliopo Kwa sasa.


"Kumekuwa na tatizo la watu kuwafuga watoto na sio kuwalea, Mtoto anaweza kurudi nyumbani muda umeenda na mzazi asiwe na habari Wala asiulize lakini  yuko tayari kuulizia mnyama kama kuku au mbuzi kucheleweshwa kurudi lakini asiulize Mtoto kuchelewa kurudi nyumbani" Alisema Kabeke.


Janga la ushoga linazidi kuongezeka na Nchi hii haiwezi kuwa na baraka kama vitendo hivyo vitaendelea badala ya kukoma ili tupate baraka zitatokana na kuwa Wacha Mungu.



Khadija Kheri ni Mmoja wa waumini waliofika katika swala hiyo ameeleza kuwa tatizo la kuchewelewa kupata Mtoto kwenye ndoa wanaume wasiengemeze Kwa wanawake peke yao kuona Wana matatizo na wengine kufata Mila potofu. 


"Tusiache swala, na Imani  potofu ni tatizo na  linawakumba watu wengi, na hii inatokana na kuacha kumcha Mwenyezi Mungu, tumrudie Mwenyezi Mungu juu ya swala" Alisema Khadija.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI