Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM MOSHI VIJIJINI ALETA FARAJA.






Na Gift Mongi ,Matukio Daima App

Moshi

Ni mwendo wa faraja kwa wasiokuwa na matumaini  kuwa chama chama cha mapinduzi(CCM)kinaenda kuleta faraja kama ilivyo dira yake!


Dira ya chama hiki kikongwe barani Afrika inaelekeza jinsi ya kuwahudumia wananchi katika nyanja mbalimbali kama inavyofanyika kwenye baadhi ya maeneo.


Leo hii katika kata ya Kilema Kati wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya moshi Vijijini na Yuvenail Shirima imefanya ziara yenye mashiko Kwa chama hicho lakini pia uhai wa jumuia hiyo.


'Ni kweli tumefanya ziara hapa Kilema Kati lakini tumefanya lengo la Ziara iliwa ni kusikiliza kero za vijana wa bodaboda na vijana mbalimbali na kuendelea kupokea wanachama wapya wa CCM'amasema


Wakongwe wa siasa wanasema Ziara hizi huenda zikaleta matunda mazuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025.


'Vijana wanakipambania chama(CCM)kama tulivyofanya sisi enzi za ujana wetu naona wataenda kufikia mbali'anasema kada wa CCM ambaye pia aliwahi kuhuudumu kama waziri kwenye serikali ya nne.


Kwa mujibu wa mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini  Yuvenail Shirima ni kuwa  ziara hizo ni miongoni mwa ziara za kata kwa kata zinazoendelea kwenye ratiba ya kamati ya utekelezaji


'Tuna mpango wa kugusa kata kwa kata sasa niwaambie hapa tunamwakilisha mama(Dkt Samia Suluhu Hassan)sisi ndio tumfikishie taarifa sasa'anasema


Gerson Kileo anasema mbali na ziara za viongozi hao katika eneo lao ipo haja ya kutafuta suluhisho la ajira  kwa vijana.


'Vijana wapo waliosoma ila changamoto ajira sasa vijana tuungane katika hili ila tushukuru kwa ujio wenu'anasema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI