Header Ads Widget

MBUNGE WA MOSHI VIJIJINI PROF. NDAKIDEMI AENDELEA KUIPIGANIA BARABARA YA KIBOSHO SHINE - KWA RAFAELI..



Na WILLIUM PAUL.

MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ameendelea kupambana Bungeni kuhakikisha barabara za Jimbo hilo zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuondoa hadha wanayaoipata wananchi wake.


Mbunge huyo amehoji Bungeni je Serikali ina mkakati gani kukamilisha barabara ya Kibosho shine hadi kwa Rafaeli kwa kiwango cha lami.


Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema kuwa, barabara hiyo inahudumiwa na wakala wa barabara nchini Tanroad lakini kipo kipande kinahudumiwa na wakala wa barabara vijijini Tarura.


Mhandisi Kasekenya alisema kuwa, kwa upande wa Wakala wa barabara Tanroad ni mpango wao kuhakikisha wanaijenga yote kwa kiwango cha lami na hadi sasa Mkandarasi yupo saiti.


Alisema kuwa, Wizara katika mwaka wa fedha 2023/2024 wametenga fedha kuendelea na ujenzi kwa awamu kwa kiwango cha lami ili kukamilisha barabara yote.


Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa kata za Kibosho ambao wanaitegemea barabara hiyo kuwaletea maendeleo yao.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS