Header Ads Widget

MABORESHO MAKUBWA KUFANYIKA JESHI LA POLISI

 


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameweka wazi baadhi ya maeneo ambayo wizara imepanga kuyafanyia maboresho makubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.


Ameeleza adhma hiyo baada ya kumaliza kutoa maoni kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande huku vyombo vilivyopo chini ya wizara yake ni miongoni mwa taasisi ambazo tume hiyo inafanyia kazi pia katika uboreshaji huo,Tume hiyo  iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo ikiwa kupitia taasisi na mifumo mbalimbali inayoshughulika na utoaji haki.


“Tunatimiza adhma ya Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo ametaka kuona maboresho katika vyombo vya utoaji haki,hasa mambo yanayosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi ambayo yamekua kero na yanaathiri haki za wananchi, kwahiyo maoni yangu niliyotoa yamelenga Zaidi kuleta mabadiliko ya kimuundo,kisheria na kikanuni na kuweza kuwa kuwa na vyombo vya polisi,magereza ambavyo havitakuwa na changamoto katika maeneo ya utendaji kazi .”alisema Waziri Masauni


“Maeneo ambayo nimetoa maoni na kama wizara tumedhamiria kuyaboresha ni eneo la Upelelezi,Ubambikizaji wa Kesi,Utoaji wa Dhamana na Mrundikano wa Mahabusu katika Vituo vya Polisi na Magereza, hayo yamekua maeneo ambayo tumekua tukipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.” Aliongeza Masauni


Katika kikao hicho waziri Masauni pia alipata wasaa pia wakubadilishana mawazo na wajumbe mbalimbali wa tume hiyo,wakiwemo Wakuu wa Jeshi la Polisi Wastaafu, Said Mwema na Balozi  Ernest Mangu huku tume hiyo ikitarajiwa kukamilisha ukusanyaji wa maoni ifikapo mwezi April mwaka huu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS