Na Fadhili Abdallah,Kigoma
VIONGOZI wa dini ya kiislam mkoani Kigoma wamekemea tabia na miendendo isiyo ya kimaadili na utu wa mtanzania ya baadhi ya wananchi wa mkoa Kigoma vya kufanya mapenzi juu ya makaburi
Mhadhiri Maarufu wa dini ya kiislam nchini, Shekhe Ibrahim Mbaruku ametoa kauli hiyo kwenye swala ya Eid Elhaj ambayo ilifanyika kimkoa kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma na kusema kuwa vitendo hivyo vinaenda kinyume na misingi na imani za dini na mila za Mtanzania.
Shekhe Mbaruku alisema kuwa katika kuelekea sikukuu ya Eid Elhaji wamekumbana na uwepo wa kondomu zilizotumika juu ya makaburi mengi katika Makaburi ya Lubengera Mjini Kigoma na kwamba jambo hilo halikualiki na kutaka wanaofanya hivyo waache mara moja
Naye Mhadhiri wa dini ya Kiislam katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye alihudhuria sala hiyo ya Eid Elhaji Mjini Kigoma, Ibrahim Sagada alisema kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa mila na desturi za kitanzania jambo linalofanya watu wngi kufanya mambo ambayo hayaendani na misingi ya dini na utamduni wa Mtanzania.
Alisema kuwa ni lazima watanzania wafuate maandiko ya dini lakini pia kufuata maelekezo ya viongozi wao na hasa katika kutunza amani, upendo na mshikamano wa watanzania wote.
Akizungumza baada ya Swala ya Eid Elhaj Kaimu Shekhe wa mkoa Kigoma,Abbasi Iddi Noboka amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kuzingatia suala la amani na usalama ili kuiepusha nchi kuingia kwenye machafuko.
0 Comments