Header Ads Widget

MAAFISA WAKAGUZI WA POLISI NJOMBE WAONGEZEWA MBINU ZA KUKABILIANA NA UHALIFU

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe John Makuri Imori

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ili kukabiliana na matukio ya kihalifu ambayo yamekuwa yakiripotiwa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini,Jeshi la polisi makao limetoa mafunzo kwa maofisa wakaguzi wa polisi mkoa wa Njombe ikiwa ni moja ya jitihada za kuwaongezea mbinu za kukabiliana na uhalifu.


Akifunga mafunzo hayo ya miezi miwili Kamishna msaidizi wa Polisi Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe John Makuri Imori amesema mafunzo hayo yatasaidia sana kuongeza umakini kwa askari katika kupambana na wahalifu.


Aidha Kamanda Imori amewataka wananchi kutambua kuwa jeshi lao liko imara katika kuwalinda wao na mali zao.


Hata hivyo Baadhi ya maofisa wakaguzi wa polisi kutoka Kata mbalimbali   mkoani Njombe akiwemo Afande Wilfred Willah,Egnatha Amani,Nassoro Mussa Omary na Afande Marwa Kisyeri wamekiri kunufaika na mafunzo hayo huku wakiwataka wananchi watarajie uimarishwaji wa ulinzi na usalama katika maeneo yao.


Kwa upande wao wakazi wa Njombe akiwemo Lusius Kawogo na Lukule Mponji wamesema matukio ya majambazi na vibaka yamekuwa yakiwarudisha nyuma kimaendeleo hivyo mafunzo hayo kwa askari yasaidie kupunguza wizi na ujambazi.


Mafunzo hayo yanayowaongezea ujuzi na mbinu mpya kwa askari polisi yamefanyika kwa awamu ya kwanza kwa nchi nzima huku yakitarajiwa kutolewa mengine kwa awamu ijayo.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI