Amina Mkumba aibuka kidedea kura za maoni Jimbo la Kibiti kwa kura 4712.
Akitangaza matokeo ya kura za maoni ya nafasi ya Ubunge jimbo la Kibiti Katibu wa CCM wilaya ya Kibiti Steve Shija amesema Amina Mussa Mkumba ameongoza kwa kupata kura 4,712 sawa na 68.5%.
Akifuatiwa na Khalid Bakari Mtaraziki aliyepata kura 1,102 sawa na asilimia 16% wakati Ally Seif Ungando amepata kura - 1,068 sawa na asilimia 15.5.
Matokeo ya kura za maoni Jimbo la Kibitl mwaka 2025 idadi ya kura zilizopigwa ni kura 7,007, kura zilizoharibika 137,
Halali ni kura 6,870.
0 Comments