Header Ads Widget

WAKULIMA MKUNWA WAFURAHIA MBEGU BORA ZA MIHOGO

 


NA MWANDISHI WETU, MTWARA


Wakulima wa zao la muhogo Wilaya ya Mtwara wamefurahia ufundishwaji wa teknolojia  katika mashamba darasa ya zao la muhogo yaliyowekwa katika Kata mbalimbali Wilayani humo.


Akizungumza wakati wa kuvuna mihogo katika shamba darasa la Kata ya Mkunwa Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi ya viazi na mihogo kutoka taasisi ya utafiti wa klimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele  Festo Masisila  alisema kuwa wanazo aina mbalimbali  za Tricas 1,2,3,4 na 5 ambazo zimedhibitishwa na Taasisi ya Tosc mwaka 2009.


Alisema kuwa kupitia mashamba darasa wakulima wamejifunza kuanzia kuandaa mashamba mpaka uvunaji na namna ya kuyabaini magonjwa  batobato kali pamoja na michilizi kahawia.


"Tuliweka shamba darasa ili wakulima waweze kuwa na machaguo kulikngana na sifa mbalimbali za mbegu ambapo mbali na Taricas pia zipo  mkumba, chereko, mkuranga, kiroba na kipusa mkulima anachagua mbegu gani inafaa Kwa biashara na chakula" alisema Masisila 



Nae Mussa Liponda afisa kilimo kata ya Mkunwa alisema kuwa TARI wamefanya jambo kubwa Kwakuamua kutuletea mashamba darasa ya mihogo.


"Wakulima wengi wameshangaa tulipanda miezi michache sana na tumepatapata mavuno mengi mbegu hizi zinafaa Kwa Kilimo biashara  sasa tunaweza kuhama kutoka kwenye mbegu za asilia  na kuanza kulima mbegu bora kwakutazama muhogo kibishara na kwa mihogo mibichi


Nae Fatuma Rambaramba mkulima wa muhogo Kata ya  Mkunwa alisema kuwa mbegu hizo zinafaa Kwa Kilimo biashara.



"Mfano mbegu ya kiroba nimeiona ni mbegu bora ukipanda mapema unavuna mapema na inajaa sana kwenye shina hivyo inakuwa mihogo mkubwa zaidi haina madoa haishambuliwi na magonjwa kama mihogo mingine" alisema Rambaramba


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI