Header Ads Widget

RC MAKALLA APONGEZA DAWASA KUPELEKA MAJI MAENEO YA PEMBEZONI



- Afanya Ziara mtaa kwa mtaa, Nyumba kwa Nyumba Jimbo la Kibamba kuthibitisha usambazaji wa Maji kwa Wananchi.


- Ampongeza Rais Dkt, Samia kuwa Suluhu ya tatizo la uhaba wa Maji Kibamba.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla amepongeza Jitiada zinazofanywa na DAWASA katika kuyaishi Maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama Ndoo kichwani kupitia Usambazaji wa Maji kwa Wananchi hususani wa pembezoni mwa mji.


CPA, Makalla amesema hayo wakati wa Ziara ya kukagua usambazaji wa Maji kwa Wananchi wa Jimbo la Kibamba ambapo ameshuhudia Na kuwasikia Wananchi wakikiri kuwa wanapata huduma ya Maji.


Katika Ziara hiyo, CPA Makalla amepokea Taarifa ya Hali ya Hali ya Upatikanaji wa Maji ambapo kwa Jimbo la Kibamba zaidi ya Wananchi 25,000 wamefikishiwa huduma ya Maji.



Aidha CPA, Makalla amemshukuru Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Suluhu ya tatizo la muda mrefu la uhaba wa Maji kwa Wananchi wa Jimbo la Kibamba kupitia ujenzi wa tank kubwa la Maji la Mshikamano.


Kutokana na Maboresho hayo, CPA Makalla ametoa wito kwa Wananchi Kutuma maombi ya kuunganishiwa Maji na kuwaelekeza DAWASA kuwa wepesi kwenye uunganishaji wa Maji.



Kwa Upande wao Wananchi wa Kibamba wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza kwa vitendo ahadi ya Kumtua Mama Ndoo kichwani ambapo wamekiri kuwa Hali ya Upatikanaji wa Maji kwa Sasa imekuwa ya uhakika.


Kwa Mujibu wa DAWASA mpaka Sasa zaidi ya kilometers 200,000 za mtandao wa mabomba yametandazwa ardhini na kazi ya kusambaza Maji inaendelea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI