Na mwandishi wetu, Lindi
Watafiti wa zao la muhogo wametoa elimu kupitia mashamba darasa ya zao hilo mkoani Lindi ili kweza kuhamsisha wananchi kuongeza uzalishaji kwakulima kilimo biashara kwakutumia mbegu bora.
Akizungumza na wakulima wa kata ya Kiwalala mkoani Lindi Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi ya viazi na mihogo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele Festo Masisila alisema kuwa walipanda mbegu aina nane katika shamba hilo ili kusaidia kupata mbegu inayofaa kwa eneo hilo.
“Yaani hapa tuliweka shamba darasa la kata na kupanda mbegu aina nane ambazo zinazaa kwa wakati ndani ya miezi 9-12 zinakuwa zimekomaa kabisa kwa matumizi yote zinavumilia magonjwa na ukame zinazaa kwa tija” alisema Masisila
Nae Benita Mkanga mkulima wa kijiji cha Mahumbika mkoani Lindi mkulima wa mihogo anasema kuwa amekuwa akitumia mbegu za kienyeji kwa miaka mingi bila kuona tija katika zao la muhogo ambapo upatikanaji wa mbegu bora unampa nguvu ya kuendelea kulima zao hilo.
“Nimetumia mbegu za kienyeji kwa muda mrefu ambazpo hakuwa na tija kwangu naamini kuwa nikitoka katika shamba darasa naenda kuboresha kilimo kwasababu naamini kuwa mbegu hii imenitoa katika sehemu moja na kuniweka katika sehemu nyingine”
Naye Mfaume Kirumbi mkazi wa Kiwalala mkoani Lindi alisema kuwa mafunzo ya watalaamu kutoka Tari Nalindele yamewapa nguvu ya kuendelea kulima zao hilo.
“Kusema kweli tulikuwa tuna mbegu nyingi tunalima lakiini kwa mbegu hizi za utafiti zitausaidia sana ipo mbegu ukipanda heka moja tu unaweza kufanya vizuri”
0 Comments