Na Mwandishi wetu, Mtwara
Kanisa la waadventisa wasabato Mtwara kati kupitia kwaya ya Hope Generation SingersTz imefanya bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha michezo na uchangiaji wa damu kwa wahitaji na upimaji wa afya katika maadhimisho ya miaka kumi ya kwaya hiyo.
Bonanza Hilo lililofanyika katika viwanja vya bonanza Mtwara lilijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa mbio za mita 100/200, mbio za magunia, miguu, kuvuta kamba, na kukimbizwa kuku kisha upimaji wa afya utakaofanyika Mei 24 na 25 katika viwanja vya kanisa hilo.
Akizungumza wakati wa Bonanza hilo mbele ya Mzee wa Kanisa la Mtwara kati David Joshua, Mwenyekiti wa kwaya hiyo Watson Mwakijola alisema kuwa bonanza hilo limeshirikisha watu mbalimbali likiwa na lengo la kuisaidia Jamii kiafya na kuhamasisha uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya watu.
“Michezo ni njia moja wapo wa kuboresha afya lakini pia tunategemea kuwa na zoezi la uchangiaji damu tunacheza ili kuhamamasisha watanzania wajitokeze kwenye kambi ya siku mbili ya upimaji wa afya itakayoendeshewa kanisani ambapo madaktari watapima magonjwa mbalibali ikiwemo presha, kisukari, hormone imbalance, na magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa pamoja na ushauri nasaha utatolewa pia”
Nae Esther Gekura mwanakwaya alisema kuwa wakati wakiadhimisha miaka 10 ya utume wa kwaya hiyo wameona vema kuisaidia Jamii kwakuhamasisha uchangiaji damu na kicheza michezo ambayo inasaidia kuimarisha afya.
“Wapo watu wengi ni wahitaji wa damu katika mahospitali yetu tena wanahitaji damu ili kuokoa maisha yao tunahamasisha uchangiaji damu ili kuweza kuwasaidia wanawake wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na watu wenye magonjwa mbalimbali pamoja na wale waliopata ajali damu ni uhai” alisema Gekura
Nae Sabato Magambo kocha ya timu ya mpira wa miguu wa kwaya hiyo alisema kuwa michezo ni afya na wataendelea kuhamasisha michezo Kwa Jamii ambayo itamsaidia kuimarisha afya.
“Leo tumecheza na timu ya kanisa la wasabato shangani tumewashinda mbili bila hii inatupa nafasi ya kuongeza bidii na kufanya mazoezi kwa wingi sio tu kushinda tena hapana tunahamashisha kucheza ili kuboresha afya zetu” alisema Mambo
0 Comments