NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza imekutana na Baraza la Taifa la Hifadhi ya usimamizi wa Mazingira na Kufanya tathimini ya namna ya kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na mifuko ya plastiki.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ameeleza kuwa kumekuwa na viwanda bubu vinavyotengeneza mifuko hiyo na vingine halali ambavyo vinazalisha bidhaa haramu ya plastiki.
Malima Amesema kuwa kutokana na mifuko hiyo ya plasitiki kuteketezwa mwaka 2019 na kufanya mabadiliko ya kanuni inayotafsiriwa vibaya na watu na kutumia mwanya huo kurejesha matumizi ya mifuko hiyo.
Ameeleza kuwa Watanzania walio wengi bado hawana elimu ya kutosheleza juu ya kuteketeza mifuko hiyo na uwepo wa baadhi ya matumizi ya plastiki hayana sababu ya kuendelea kuwepo.
"Unakuta mtu unafungia ndimu, vitunguu, pikipiki, nyanya na karoti kwenye mifuko ya plasitiki wakati hitu hivyo mtu anaweza kubebea kwenye vifungashi vilivyoruhusiwa"Alisema Malima.
Hamadi Taimuru Meneja Uzingatiaji wa sheria NEMC Taifa ameeleza kuwa wanatarajia kuanza ukaguzi Kwa ajili ya kuwakumbisha wananchi waliojisahau na wanaofanya makusudi juu ya matumizi mabovu ya plasitiki na utumiaji wa mifuko Mbadala.
Taimuru Amesema kuwa Kuna ulazima wa wananchi kuteketeza kanuni na sheria zinazopiga marufuku bidhaa zilizokataliwa.
"Lazima tujue tatizo la mifuko ya plasitiki limekatazwa na ikaruhusiwa vifungashio Kwa baadhi ya bidhaa kama vile njegere, pikipiki, vitunguu, karoti ambavyo ni lazima viwe kwenye mifuko Mbadala iliyopitishwa" Alisema Taimuru.
Amefafanua kuwa plasitiki Ina kemikali ambayo ni hatari Kwa afya ya binadamu inapaswa Kila mmoja kujitahidi kutotumia bidhaa ambazo haziitajiki na hazisitahili hususani vifungashio vya plasitiki.
" Lakini kama tunataka afya ya mwanadamu na mifungo kuwa salama ni lazima tuwe makini, tumeweza kuona picha namna ndege amejivisha Mfuko wa plasitiki na akikosa mtu wa kumtolea anafariki hivyo hivyo hata Kwa watoto wetu wanaotumia vifungashio hivyo vyaplasitiki kwenye barafu" Alisema Taimuru.
Kwa upande wake Meneja Kanda ya ziwa NEMC Jarome kayombo ameeleza kuwa Kuna sheria, kanuni ya mazingira ambayo inapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plasitiki, ambapo kanuni hiyo imeanisha adhabu ya makosa mablimbali itokanayo na uvujifu wa kanuni.
Kayombo ameeleza kuwa mtu yeyote atakaye kamatwa anayejihusisha na uzalishaji, uwingizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya Nchi, msafirishaji kwenda nje ya Nchi pamoja na wasambazaji wa mifuko hiyo ya plasitiki atachukuliwa hatua na kulipa faini, au kifungo Cha miaka miwili na wakati mwingine kutumikia kifungo na faini Kwa pamoja.
0 Comments