Header Ads Widget

MBIO ZA MWENGE ZAZINDUA KITUO CHA MAFUTA CHA KISASA MAFINGA

 





Na RAYMOND MINJA MATUKIO DAIMAAPP, MAFINGA


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Abdala Shaibu  Kaim ameweka jiwe la msingi katika kituo cha mafutu cha  Njombe Filling Tastion ( NFS) cha mjini Mafinga kitakachogarimu kiasi cha shilingi  milioni 850,000,000.


Kukamilika kwa kituo hicho cha mafuta ambacho kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo vilainishi vya Magari kitatoa ajira zaidi ya watu 30 ambo wanufaika wake ni wakazi wa mafinga .


Akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Abdala Shaibu Kaima imepongeza mwekezaji wa kituo hicho James Mwinuka kwa kuwekeza katika mjii huo wa kibishara kwani kituo hicho kitasaidia kukuza uchumi wa watu wa mafinga.


Kaim amesema kuwa Serekali imepanua wigo wa wekezaji nchini ili kuendelea kufungua fursa za kibiashara nchini jambo ambalo pia ni faida kwa serekali kwani itakuwa ikiongeza mapato yake.


"Niwapongeze sana kwa uwekezajii huu mkubwa ,mbio za mwenge zimeridhishwa na mradi pamoja na nyaraka zake zote hivyo tuko tayari kuzingua kituo hicho asanteni sana na hongereni kwa kufungua fursa mafinga."


kwa upande wake mbunge wa Mafinga Mji Cosato Chumi aliwapongeza wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza katika mji wa kibiashara mafinga na kufungua fursa kwa watu wake.


Chumi alisema kuwa kufunguliwa kwa kitoa hicho licha ya kutoa ajira kwa watu wamafinga bali ni faida kwa Serekali itapata faida kwa kukusanya kodi.


"Miakaa michache hapo nyuma mzee mwinuka alitualika kule njombe kwenye uzinduzi wa kituo kama hichi,nikamwambia mzee mwinuka embu sogea na mafinga tulete huduma hii,hatimaye leo lile nililomwambia limetimia niwashukuru sana" . Chumi Mbunge 


Awali akisoma risala ya uzinduzi huo Daudi Mwinuka alisema  kuwa lengo la kujenga kituo hicho ni kutoa  huduma bora ya mafuta na vilainishi kwa ajili ya magari na mitambo kwa wakazi wa mji wa Mafinga pamoja na wasafiri na wasafirishaji wanaopita barabara kuu ya Iringa -Mbeya.


Hata hivyo David ameshukuru serekali ya awamu wa sita chini ya uongozi thabiti wa mh Dkt  Samia Suluh Hassan Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wazawa kuweka shughuli za uwekezaji

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI