Header Ads Widget

BILIONI 4.5 KUMALIZA KERO YA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI VIJIJI 10 MTAMA

 


NA HADIJA OMARY LINDI.



Hatua ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi biloni 4.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji ukanda wa Navanga Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi  kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa  imetajwa kumaliza kero hiyo kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) Wilaya ya Lindi, Mkuu wa Wilaya hiyo Shaibu Ndemanga alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maji katika Wilaya hiyo ya Lindi..



Ndemanga alisema Mpaka sasa Serikali ya Rais Samia kwa Wilaya ya Lindi pekee imeshatoa Zaidi ya shilingi bilioni 14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maji ambapo mpaka sasa upatikanaji wa huduma hiyo umefikia asilimia 76.




“sisi wilaya ya Lindi , kila  Kijiji tunayo miradi mbali mbali  inayotekelezwa ambapo ikikamilika tunamatumaini ifikapo mwaka 2025 inawezekana hatutakuwa na Kijiji ambacho hakina maji kwani kwa hivi sasa miradi yote mikubwa tunayoianzisha inaenda kuunganika na miradi midogo midogo ambayo ilikuwa inafanya kazi ili kuongeza uwezo wa upatikanaji wa maji”.



Kuhusu mradi huo wa Maji wa ukanda wa Navanga Ndemanga aliwaagiza RUWASA kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kadri unavyoendelea kulingana na Vijiji vinavyofikiwa na Mradi badala ya kusubili kukamilika kwa vijiji vyote vilivyopangwa..



“ Tulikubaliana huu mradi unatekelezwa kwenye vijiji 10 sasa ule utaratibu wa kwamba mradi mpaka unaisha mpaka Kijiji cha mwisho ndo mradi unaanza kutumika huo tumeshaachana nao,.



“Mradi huu ukianza hapa bomba likifika simana  na watu wa simana waanze kupata maji  mkiendelea mkifika Nampunga watu wa Nampunga wapate maji  kwa hivyo  iendelee hivyo hivyo kwa vijiji vyote na mtakapofika Kijiji cha mwisho sasa ndio tutafanya uzinduzi”.



Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji  Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Lindi Mhandis Iddi Pazi alisema Mradi huo wa Ukanda wa Navanga unatekelezwa na Mkandarasi Helem contruction company limited ambao kwa sasa umefikia asilimia 60% ya utekelezaji wake na kwamba unatarajiwa kukamilika mwezi July mwaka 2023.


“Mradi huu kwa sasa   umefikia asilimia 60 ya utekelezaji wake na  kazi zinazofanyika hivi sasa ni ulazaji wa mabomba wa km 84 ambapo kwa sasa tumeanza kulaza mabomba kutoka hapo Kijiji cha mnali kuja huku kwenye tank na tumeshalaza na kuunda mabomba kwa mita nane  na kazi inaendelea  kutoka Kijiji cha mnali kuja  kwenye tanki”

 



Alisema  baada ya kukamilika kwake  Mradi huo unatarajiwa kuhudumia vijiji 10 vya ukanda huo ambavyo ni mongomongo, nampunga, navanga , sudi A na B , kilimani, mmumbu, Nachunyu, simana pamoja na mnali.


Hata hivyo Mhandisi Pazi alieleza kuwa  ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa ukanda huo kwa sasa ni asilimia 0% huku uzalishaji wa maji baada ya mradi kukamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita laki tano huku mahitaji yakiwa lita laki tano kwa siku.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI