-Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 6 na kukimbizwa umbali KM 128.5
Mwenge wa Uhuru 2023 Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam umekimbizwa umbali wa KM 128.5 na kukagua miradi 6 yenye thamani ya Tsh.Bilioni mbili laki tisa laki nane na themanini na tano elfu laki tisa na elfu arobaini.(2,900,885,940.48), miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru, hakuna mradi uliokataliwa.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge huo ni Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Tungi- Mji mwema (0.35 KM), Ujenzi wa kituo cha Afya Kibada, Utunzaji wa Mazingira kwenye Vyanzo vya Maji Kisarawe II, Mradi wa Utunzaji wa mikoko Tundwi Center.
Mradi wa Kilimo cha nyanya kikundi cha vijana na Kilimo na mradi wa ujenzi wa Chuo cha maendeleo ya wananchi Arnautoglu Kigamboni.
Mwenge wa Uhuru 2023 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam leo Mei 26, 2023 umekabidhiwa Wilaya ya Ilala unatarajia kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
0 Comments