Header Ads Widget

MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI TISA YAZINDULIWA, KIGAMBONI




Licha ya kuwa Wilaya changa lakini katika muda wa miaka mitano Kigamboni imeweza kutekeleza miradi mbalimbali na kwa muda mfupi.


Hayo yamethibitishwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Dkt, Faustini Ndungulile mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru2023, Ndg. Abdallah Shaibu.


Amesema Wilaya ya Kigamboni ni miongoni mwa Wilaya changa, lakini ni Wilaya inayokuwa kwa kasi kwa mfumo wa 5G.


“Ndani ya miaka 5, tumejenga Ofisi ya Halmashauri, Jengo la Mkuu wa Wilaya, Hospitali ya Wilaya, nyumba za Watumishi na Makao Makuu ya Polisi” alisema Mbunge.


Pia ameongeza kuwa kukamilika kwa Chuo cha FDC ni moja ya mikakati ya kukuza elimu katika wilaya yetu ya Kigamboni.


“Chuo hiki ni kipya kama nilivyosema kwenye risala  chuo hiki kitakwenda kutoa fursa kwa wakazi wa Kigamboni  kupata fursa mbalimbali za masomo, Kigamboni ni Wilaya tunayo fanya vizuri sana na tupo vizuri sana” alisema Ndungulile.


 Jumla ya miradi 6, yenye thamani ya shilingi bilioni 9 katika Wilaya ya Kigamboni imekaguliwa na kuzinduliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru2023, Kitaifa Ndg. Abdallah Shaib.


Wakati akiwa katika maeneo ya miradi amesisitiza wananchi kuzingatia kaulimbiu ya mbio za Mwenge kwa mwaka 2023 inayosisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji, kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa.


Pia kiongozi huyo aliitaka jamii kupiga vita rushwa na  kuhimiza lishe bora, kupambana na ugonjwa malaria pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amesema katika miradi iliyozinduliwa na kukaguliwa ipo iliyokamilika na mingine iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


"Miradi hii ikiwemo ujenzi wa barabara, vituo vya afya, na miradi ya maji ni miradi inayotekelezwa na fedha za ndani, zipo fedha zinazotoka Serikali Kuu na nyingine kwenye halmashauri," amesema Bullembo 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI