Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAZINDUA BARABARA YA LAMI YA GENGERANKURU-MOMA WILAYANI MKALAMA

 

Na Thobias Mwanakatwe,MKALAMA

MWENGE wa Uhuru 2025 umeridhia na kufunga barabara ya Gengerankuru-Moma yenye urefu wa mita 640 ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami kwa thamani ya Sh.milioni 597.119.


Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Mhandisi Rahabu Thomas,akitoa taarifa leo ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025,Ismail Ali Ussi, alisema barabara hiyo ujenzi wake ulianza Agosti 20, 2023 na kukamilika Juni 16, 2025.


Alisema barabara hiyo ambayo imejengwa na mkandarasi JP Traders Ltd ambapo katika awamu ya kwanza kazi zilizofanyika ni ujenzi wa kitanda cha barabara,tabaka la kwanza na la pili la udongo,uwekaji wa lami nyepesi ,ujenzi wa tabaka la juu,uwekaji wa taa 10 na ujenzi wa mfereji kilometa 0.64.


"Awamu ya pili M/S Valee Builders &enterprises Ltd na M/S Ngachenga  Co.Ltd walikamilisha ujenzi wa mfereji na kingo za tuta la barabara,uchoraji wa mistari ya alama barabarani na uwekaji wa taa 12 za barabarani," alisema Thomas.

Mhandisi Thomas alisema faida ya mradi huo ni pamoja na kurahisisha huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Mkalama wanaokwenda kupata huduma katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kutoa ajira za muda kwa watu143.

"Sisi wananchi wa Mkalama tunamshukru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwani katika uongozi wake wa awamu ya sita kwa kutupatia fedha Sh.9,250,400,000 za kutekeleza miradi ya barabara katika Wilaya ya Mkalama," alisema.

Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi,aliishukru TARURA kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitengeneza na kuboresha barabara za mijini na vijijini.

"Kwa kipekee nikushukru Meneja wa Wilaya na Meneja wa Mkoa TARURA kwa jinsi mnavyofanya kazi vizuri za ujenzi wa barabara  na kuwarahisishia wananchi usafiri," alisema Ussi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI