Na Matukio Daima Media,Mbeya
UWEPO wa mbio za Tulia Marathon mkoani Mbeya zimeelezwa kuchochea fursa za kiuchumi kwa wafanyabishara kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka mikoa mbalimbali na raia kutoka nchi jirani ya Kenya.
Diwani wa Kata ya Majengo na Mwenyekiti wa Chama cha riadha Mkoa wa Mbeya ,Maulid Jemedali wakati akizungumza na Matukio daima amesema hayo leobkatika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya ikiwa ni siku ya kwanza ya mashindano hayo.
Jemedali amesema kuwa uwepo wa mbio hizo umekuwa chachu ya kuchangia shughuli miradi ya Maendeleo ya Serikali ikiwepo sekta ya elimu na afya jambo ambalo inaongeza tija katika utoaji huduma bora kwa jamii.
"Kwa Jiji la Mbeya tunaona mambo mengi ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika Sekta ya elimu na afya yanafanywa kupitia fedha zinazopatikana kupitia mashinsano ya mbio za Tulia Marathoni "amesema.
Joshua Mwakanolo ni Ofisa habari na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust amesema kuwa Mbeya Tulia marathon lengo lake kubwa ni kuboresha miundombinu ya elimu na afya na kwamba huo ni msimu wa saba toka kuanzishwa kwa Mbeya Tulia Marathon.
‘’Kwa kumbukumbu kwa mwaka 2022 Mbeya Tulia Marathon fedha iliyopatikana ilipelekwa kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari ipinda wilayani Kyela baada ya hapo yalijengwa madarasa mawili shule ya sekondari Lyoto pamoja na ofisi ‘’amesema.
Ameongeza kuwa ‘’Hata mwaka huu tunategemea kwamba fedha itakayopatikana tutaangalia jinsi gani tunaweza kujigawa ili kuweza kuboresha miundo mbinu ya afya na elimu sababu tunaona kuna mwitikio mkubwa hata uandikishaji kwani kati ya watu 4,000 waliojitokeza 14,kutoka nchi jirani ya Kenya’’ amesema.
Amesema kuwa mashindano hayo yamekuwa na mchango mkubwa sana kwa jamii hususan kuchangia ukuaji wa kipao cha mtu mmoja mmoja na vikundi wakiwepo wafanyabishara wa viatu,nduo,mama lishe na wauzaji wai vileo’’amesema
Tulia marathon imekuwa msaada mkubwa kwa wajasiliamali wa mkoa wa Mbeyakwani itaweza kukuza uchumi.
Sophia Mwanautwa ni Diwani wa vitimaalum Kata ya Makongolosi amesemakuwa lengo kuu la tulia marathon ni kuboresha elimu na afya hivyo spika wa Bunge amekuwa akipenda maendeleo na akizungumzia elimu na anafanya kwa vitendo.
Mh. Mwanauta amesema kubwa wana Mbeya wanapoona Mh. Spika anafanya jambo wamuunge mkono na kumpa sapoti ili aweze kufanya vitu vya maendeleo.
‘’Kwasababu kujiandikisha sio lazima ukimbie mbio mimi hapa nimejiandikisha nakimbia kilometa tano(5) na namba yangu ni 0368 sio kwamba kesho nitakimbia ila nimechangia kumsapoti Mh. Spika na mbunge wa jimbo la Mbeya , nawaomba wana chunya mwakani wajitokeze kwa wingi ili kumuunga mkono mwana mama huyu katika juhudi zake za kuboresha elimu kwa mkoa wa Mbeya’’amesema Mh. Diwani huyo.
0 Comments