ZAIDI ya madereva malori na mabasi 200 katika mkoa wa Iringa wamerejeshwa darasani kunolewa zaidi juu ya sheria za usalama barabarani kama mkakati moja wapo wa kupunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na baadhi ya madereva waio na weledi wa kazi hiyo .
Akifungua jana mafunzo hayo ya udereva ya wiki mbili yaliyoandaliwa na chuo cha Ufundi stadi VETA mkoa wa Iringa kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi alisema kuwa Taifa linashtushwa sana na matukio ya ajali za barabarani zinazotokea hususani za mabasi ,malori na magari mengine yanayobeba abiria hivyo kupitia mkakati huo wa kuwarudisha darasani] madereva utasaidia kupunguza ajali .
Alisema kuwa ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva na kuwa pamoja na juhudi kubwa za jeshi la polisi na wasimamizi wengine wa sheria kuendelea kutoa elimu ,kuonya na kufanya oparesheni mbali mbali bado jeshi la polisi mkoa wa Iringa litaendelea kuchukua hatua kali na madhubuti za kukabiliana na hali hiyo ya ajali .
Bukumbi alisema ajali nyingi zimekuwa zikicvhangiwa na sababu mbali mbali kama maddereva wa magari na pikipiki kuwa sehemu kubwa ya vyanzo vya ajali kwa kutiozingatia sheria kwa kuendesha kwa mwendo kasi bila kujali ukomo wa mwendo elekezi wa kisheria ,kuyapita magari ya mbele yao bila kuchukua tahadhari,kuendesha magari mabovu barabarani pamoja na kuendesha vyombo hivyo vya moto bila kupata mafunzo katika vyuo vya udereva na baadhi yao kutokuwa na leseni za udereva .
Hata hivyo alisema kuwa kupitia mpango huo wa serikali kutaka madereva wote kurudi vyuo ili kupata mafunzo ya udereva ni wazi utasaidia sana kupunguza ajali kwa kuwa na madereva wenye sifa za vyuoni vya udereva .
" Chuo hiki cha VETA kina wakufunzi mahiri ambao tunaamini kwamba watawapika vizuri na mtaiva vizuri kwa wale ambao mtazingatia masomo yote ya darasani na vitendo " alisema Bukumbi
Mratibu wa mafunzo hayo Edmund Enugu alisema kuwa jumla ya madereva 200 wa malori na mabasi ya abiria wameanza mafunzo hayo ya wiki mbili na kuwa baada ya mafunzo hayo watapanda madaraja ya awali na kufikia madaraja ya juu ya kuendesha magari ya abiria na mizigo (PSV na HGV) .
Kwa upande wake mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini Suzana Magani alisema kuwa chuo hicho kimeendelea kutoa mafunzo ya udereva na mafunzo mengine na kutoa wito kwa wale wanaohitaji kupatiwa mafunzo mbali mbali kuendelea kujiunga na vyuo vya VETA ili kupata ujuzi kamili .
0 Comments