Header Ads Widget

KINACHOUA BIASHARA ZA MACHINGA CHABAINISHWA

 

Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali (kulia) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari akieleza kuanza kwa maonyesho ya program na mifuko ya uwezeshaji yaliyoanza mjini Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mfuko wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC) umeeleza kuwa kutofanyika kwa tafiti ya biashara mbalimbali zinazoanzishwa imekuwa changamoto kubwa kwa wajasiliamali wengi nchini na kusababisha biashara zao kufa.

 

Katibu Mtendaji wa NEEC,Being’I Issa alisema hayo akitoa taarifa ya kuanza kwa maonyesho ya sita ya mifuko na program ya kuwezesha wananchi kiuchumi yaliyoanza Mei 21 mjini Kigoma  ambayo yatafungwa Mei 27 mwaka huu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.



Issa alisema kuwa wajasiliamali wengi wa chini na wa kati waanzisha biashara kwa kuona mjasiliamali mwingine akifanya biashara hiyo bila kufanya utafiti wa wapi mali ghafi na masoko ya biashara inapatikana na bila kujua wateja wanataka nini kwenye biashara anayoanzaisha.


 

Sambamba na hilo alisema kuwa wajasiliamali wengine wamekuwa wakichukua mikopo na kuanzisha biashara bila kuwa utaalam wa biashara anayoanzisha wala kujua undani wa mambo mbalimbali ya biashara husika na hivyo biashara inapokufa inakuwa changamoto kubwa katika kurudisha mikopo.




Akizungumzia kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo kwa sasa ni mwaka wa sita mfuliulizo Mtendaji huyo wa NEEC alisema kuwa maonyesho hayo yamekuwa  na tija kubwa katika kuinua shughuli za kiuchumi za wajasiliamali wanawake nchini.

 

Alisema kuwa kwa miaka mitano ambayo maonyesho hayo yamefanyika idadi ya wanawake waliojitokeza kuanzisha biashara, kukuza biashara zao kwa kuchukua mikopo kwenye taasisi mbalimbali za fedha na mifuko imeongezeka na kufikia asilimia 70 kwa nchi nzima na kwa sasa idadi kubwa ya wanawake wanajishughulisha na shughuli za kiuchumi ikiwemo ujasiliamali.



“mkoani Kigoma maonyesho yanafanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre na yatafungwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambapo siku ya mwisho ya kufunga maonyesho kuna mikopo mikubwa inatolewa ikiwemo mkopo wa trekta kwa vikundi vya wakulima,”Alisema Katibu Mtendaji wa

 

Akitoa taarifa  katika mkutano huo na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya Kigoma,Salum Kalli alisema kuwa kufanyika kwa maonyesho hayo mkoani Kigoma kuna faida kubwa kwaoa na hasa wakati huu ambao serikali imeufanya mkoa huo kuwa wa kimkakati kiuchumi.

Akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma katika mkutano huo Kalli alisema kuwa kwa sasa mkoa Kigoma unafunguka kiuchumi hivyo kufanyika kwa maonyesho hayo kutatoa fursa kwa wananchi wa mkoa huo kujifunza na kupata taarifa ya wapi wanaweza kupata fedha na uwezeshaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara zao.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI