Header Ads Widget

WAJUMBE CCM KIGOMA KUTEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa wilaya Kigoma Salum Kalli ametangaza azma ya kuwapeleka na kuwatembeza kwenye miradi ya kimkakati wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya Kigoma Vijijini waweze kuwa na taarifa sahihi za miradi hiyo ili waweze kueleza kwenye majukwaa namna serikali inayofanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

 

Mkuu huyo wa wilaya Kigoma ameatangaza hayo wakati wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM ya wilaya Kigoma muda mfupi baada ya kuwasilisha taarifa ya utendaji inayoelezea utekeleza wa ilani ya CCM ya utekelezaji miradi ya maendeleo ya wananchi.



Kalli alisema kuwa katika wilaya hiyo ipo miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inatekelezwa kwa fedha za serikali kuu ikiwepo mikopo ya riba nafuu lakini haiku katika nafasi ya wajumbe hao kuitembelea na kwa hali hiyo sehemu kubwa ya wajumbe hao hawajawahi kufika kwenye miradi hiyo zaidi ya kusikia taarifa zake.

 

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndenge wa Kigoma ambapo kuna mradi wa kuongeza njia ya kurukia ndege, jengo la abiria na ofisi za watendaji wa mamlaka zinazopaswa kuwepo uwanjani hapo.


Mkuu huyo wa wilaya aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na ujenzi wa meli mbili mpya, ukarabati wa meli ya Mv.Liemba, Mt. Sangara na Mv. Mwongozo Sambamba na mradi wa ujenzi wa cherezo ya kutengenezea na kukarabati meli.

 

“Miradi hii yote ipo kwenye wilaya ya Kigoma ambalo ni eneo langu hivyo nimeazimia kuwatembeza wajumbe hawa waione na kuijua miradi hiyo sambamba na miradi ya barabara za kiwango cha lami, hili litawapa fursa na nafasi kubwa ya kuizungumzia miradi hiyo kwenye majukwaa mbalimbali,”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Wakizungumzia hali hiyo ya Mkuu wa wilaya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya Kigoma Vijijini walisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama kuwachukua wajumbe kwa gharama zake na kuwatembeza kwenye miradi ikiwemo miradi hiyo ya Kimkakati.

 


Mmoja wa wajumbe hao Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Kigoma Vijijini, Kasongo Abdicheko alisema kuwa ziara hiyo itakuwa darasa kubwa kwao kuijua miradi hiyo lakini kuisemea namna Raisi Samia anavyopeleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.

Naye Mjumbe wa hlmashauri hiyo ya wilaya,Angelina Kebero alisema kuwa amekuwa kwenye nafasi mbalimbali kama hizo kwa muda mrefu haijawahi kutokea kwa kiongozi kama huyo kuwapeleka kwenye miradi kama hiyo zaidi ya kutembelea miradi yao iliyopo chini ya halmashauri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI