Header Ads Widget

UVCCM MKOA WA NJOMBE KUZINDUA KAMPENI YA''NASIMAMA NA MAMA''.


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Njombe imetangaza kwenda kuzindua rasmi kampeni maalum ya kumuungano mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa majukumu anayoyatekeleza katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.


Kampeni Hiyo itakayokwenda kwa jina la Nasimama na Mama itazinduliwa Mei 2 mwaka huu na  itazunguka  mkoa mzima kwa kuzungumzia maendeleo yanayotekelezwa pamoja na kufanya mijadala na midahalo mbalimbali.


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Njombe Samuel Mgaya amesema kampeni hiyo itahusisha makundi mbalimbali ya vijana Wakiwemo wasanii ambao tayari wametunga wimbo unaoitwa Nasimama na Mama na utazinduliwa hivi karibuni.


Aidha bwana Mgaya amesema mikopo ya vijana inayotolewa na Halmashauri zote nchini wanataka ikawe na tija kwa vijana kwa kuwahamasisha kuitumia vyema Ili iwanufaishe katika maisha yao.


Hata hivyo amesema hawako tayari vijana kuwa chawa wa Viongozi huku wakikana kuwafumbia macho Viongozi wabadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo na kwamba ni wajibu wao kukabiliana na changamoyoyote  yanayotendwa na watendaji wa serikali na kukwamisha jitihada za Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo.


Katibu wa UVCCM mkoa wa Njombe Ally Hamis Kachinga naye anasema hawatovumilia maovu yanayofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali waliopewa dhamana ya kuwatumikia watanzania kwa kuharibu kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI