Na Amon Mtega _Mbinga
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Joseph Mdaka ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kigonsera kwa mshikamano wanaouonyesha dhidi ya Chama cha CCM na Serikali pamoja na Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Pongezi hizo amezitoa kwenye Mahafali ya 24 ya kidato cha sita katika shule hiyo huku wahitimu wakiwa 463 ambapo mwenyekiti huyo amekuwa mgeni rasmi.
Akizungumza kwenye mahafali hayo Mwenyekiti huyo amesema uongozi wa Shule hiyo ambayo ni Kongwe na yenye historia ya baadhi ya viongozi mbalimbali kusoma hapo kama Hayati Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu Waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera umekuwa na ushirikiano mzuri katika nyanja zote.
Mdaka ambaye amechangia Sh.Laki tano (SH.500,000=) kwaajili ya muendelezo wa ujenzi wa Nyumba za walimu unaofanyika shuleni hapo kwa kushirikiana na Wazazi ambapo hadi sasa Nyumba sita zimejengwa na malengo ni kufisha Nyumba 12 .
Aidha Mdaka amewataka wazazi kuendelea kushikamana na uongozi wa Shule hiyo bila kukata tamaa ili shule izidi kudumisha historia yake kwa vizazi na vizazi.
Kwa upande wake mkuu wa Shule hiyo Ponsiano Ngunguru ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuzijali shule Kongwe hapa Nchini ili kulinda hadhi ya shule hizo.
Ngunguru akisoma taarifa ya shule amesema kuwa kulikuwepo na majengo yaliyopoteza ubora wake (Uchakavu)lakini Serikali imeyakalabati na kuyafanya yarudi kwenye muonekano.
Akizugumzia suala la taaluma amesema shule hiyo imekuwa ikifaulisha kwa asilimia zaidi ya 90 ambao wanafunzi hao wamekuwa wakienda vyuo vikuu kuendelea na masomo yao.
0 Comments