Header Ads Widget

RC RUVUMA AWATAKA WAZAZI KUENDELEA KUSIMAMIA MAADILI KWA WATOTO



Na Amon Mtega,_Mbinga


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Rabani Thomas amewataka wazazi wa Mkoa huo kuendelea kusimamia maadili kwa watoto ili kulinda heshima ya Taifa letu.


Mkuu huyo ameutoa wito huo alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya kwanza ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Mkinga inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM .


Kanali Rabani akizungumza kwenye Mahafari hayo amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumeibuka viashiria visivyofaa kwa watoto hasa wa kiume kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja jambo ambolo lileta picha siyo nzuri kwa taifa letu.




 Aidha mkuu huyo ambaye kwenye mahafari hayo amefanya kazi mbalimbali ikiwemo ya kupanda mti kwenye eneo la shule hiyo kuzindua jengo la utawala pamoja na kukagua maeneo ya shule ,licha ya kuwataka wazazi hao kuendelea kusimamia maadili lakini bado amewaasa wanafunzi wanaohitimu kwenda kuwa mfano bora kwenye jamii kwa kujiepusha na vitendo viovu.



 Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondari ya Mkinga Jacob Msingwa awali akisoma taarifa ya shule hiyo amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye taaluma na kuwa wahitimu 33 wa kidato cha sita ambao ndiyo mahafari ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita watafaulu vizuri kwa kuwa wameandaliwa ipasavyo.



 Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbinga mkoani humo Joseph Mdaka amesema kuwa shule hiyo ni moja kati ya shule nzuri katika Wilaya ya Mbinga hivyo wazazi wasisite kuwapeleka watoto wao kwenye shule hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI