Header Ads Widget

SHEIKH SULEIMAN MAGOTI AKEMEA MASUALA YA USHOGA

Na Shomari Binda-Musoma

SHEIKH wa Wilaya ya Musoma,Suleiman Musa  Magoti,amekemea vitendo vya vijana kujiingiza kwenye masuala ya ushoga.

Kauli hiyo ameitoa leo mara baada ya swala ya Ijumaa kwenye Msikiti mkuu uliopo mjini Musoma.

Amesema umekuwepo upungufu mkubwa wa maadili kwa vijana na wanakwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu.

Amedai vitendo vya ushoga vimekuwa vikikemewa mara kadha lakini bado inaonekana vinaendelea na sauti zinapaswa kupazwa kuwakemea vijana.

Sheikh Suleiman amesema Mufti wa Tanzania amekuwa akitoa makemeo juu ya vitendo hivyo na kudai ni jukumu pia la kila kiongozi na jamii nzima.

Amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwa na muda wa kuzungumza na watoto juu ya maadili ikiwemo kukemea ushoga.

" Ndugu zangu lazima tisimame imara kukemea vitendo vya ushoga maana hali imekuwa mbaya kwa vijana juu ya ushoga.

" Maadili yameshuka tusipofanya jitihada za kukemea sisi kama viongozi na jamii tutakuja kuulizwa siku ya kiama",amesema.

sheikh Suleiman amesema waislam wilaya ya Musoma wamekusudia kuandaa kongamano juu ya maadili ikiwemo kukemea vitendo vya ushoga.

Amesema kijana anapokuwa na maadili mema huwezi kujiingiza kwenye vitendo vya ushoga kama ambavyo vinazungumziwa kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI