Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kigoma imesema kuwa serikali isipokusanya mapato haitaweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi wala kutekeleza miradi ya maendeleo.
Meneja wa mamlaka hiyo mkoani humo Bw Deogratias Shuma wakati akiongea na wanafunzi pamoja na wanachama wa klabu ya walipa Kodi (Tax clab) ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kigoma Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati akikabidhi misaada ya aina mbalimbali za juice kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Shuma alisema kuwa msingi wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake ni kukusanya mapato ya ndani ya kutosha na hata mikopo na misaada kutoka nje inawezesha kusaidia serikali inapoishi ambayo nayo pia inasisitiza ukusanyaji wa maapato ya ndani hivyo wananchi wanalo jukumu kubwa la kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali.
Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali (kulia) akikabidhi msaada wa juice mbalimbali kwa Mlezi wa kituo cha watoto Sanganigwa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo imetolewa na TRA kigoma
Kutokana na hilo alisema kuwa kulipa kodi kwa hiari sambamba na kudai na kutoa risiti wananchi wanapofanya manunuzi lazima yazingatiwe na kusimamiwa kwa karibu na watu wote na kwanza wananchi wanapaswa kuwa wa kwanza kutoa taarifa za vitendo vya ukwepaji kodi vnavyofanywa na watu wasio wema kwenye maeneo yao.
Awali Mwenyekiti wa klabu ya kodi ya Kigoma Sekondari, Safari Fredrick alisema kuwa hadi sasa klabu ina wanachama 115 huku ikifanikiwa kutoa elimu ya uzalendo wa kulipa kodi mbalimbali katika maeneo ya shule na nje ya shule hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Dickson Sisso amesema shule ya Sekondari Kigoma imekuwa mfano wa kuzalisha wasomi wenye maadili na walioiva katika fani ya uongozi na kulitumikia Taifa na kuomba ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kuisaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto zilipo shuleni hapo.
Sisso amesema kuwa shule hiyo yenye Kidato cha Tano na Sita inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi na mali zao sambamba na shule hiyo kutokuwa na ukumbi wa mikutano na mihadhara licha ya kuweka changamoto hizo kwenye mipango yao na ukosefu wa fedha unawafanya kushindwa kutekeleza mipango hiyo.
Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo kwa Jumuia ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kigoma, Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Salum Kalli amewataka wanafunzi katika shule hiyo kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu na utii kwa kuwa ndio msingi wa mafanikio katika masomo yao.
Mkuu huyo wa wilaya ametakaia mafanikio na mtihani mwema wanafunzi wa kidato cha sita wanaoanza mitihani yao ya mwisho Jumatatu huku akieleza kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji kushughulikia changamoto zinazoikabili shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1962 ikiwa shule pekee ya sekondari mkoani Kigoma kwa muda mrefu.
0 Comments