Header Ads Widget

DC BUKOMBE AJITOLEA KUHAMASISHA WAKULIMA WILAYANI HUMO KULIMA KARANGA

 





Na Mwandishi wetu, Bukombe


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkuba amesema kuwa  amejitolea kuhamasisha ulimaji wa karanga katika wilaya hiyo baada ya kulima na kuona faida yake kiuchumi.


Kauli hiyo ameitoa leo alipotembelewa na watafiti wa Zao la Karanga kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele ambapo walifika kuona majaribio ya mbegu yaliyowekwa katika Wilaya hiyo,


Alisema kuwa wilaya hiyo ina ardhi nzuri yenye rutuba hivyo inafaa kwa kilimo cha karanga kwakuwa karanga hazihitaji mbole wala viwatilifu ambapo wakulima wakielimishwa wanaweza kufanya vizuri zaidi shambani.


“Niko tayari kufanya uhamasisha wa zao la karanga katika wilaya yangu ili kuwezezsha wakulima kulima kwa wingi zaidi wakulima wengi walishaachaga kulima zao hili kikubwa inahitajika elimu na mbegu ambapo naamini kuwa watalaamu wanaweza kujitoa na kuja kukutana na wakulima na kuwapa elimu stahiki”


“Nitawaunga mkono pale mtakapo hitaji uwepo wangu kwakuwa mimi ni mkulima mzuri wa hili Napata pesa nyingi kwakulima karanga naamini kuwa wakulima wakisimama na kuamua kulifanya kama zoa la biashara wanaweza kufanya vizuri zaidi” alisema Dc Nkumba


Naye Obeid Manweli mkulima wa Karanga kutoka katika kijiji cha Ryambamgongo Wilaya ya Bukombe  alisema kuwa mbegu za majaribio zimewapa ujuzi mkubwa kupitia mashamba darasa.



“Tumepata ujuzi ambao utatuboreshea kilimo hiki lakini pia tumepata na mbegu bora za majaribio ambazo zimetupa hamasa ya kulima zaidi hata wakulima wengine wamevutiwa kupanda mbegu bora sio tu kwa mwonekano shambani bali zimekuwa na matokeo chanya”


Kwa upande wake Afisa Kilimo Kata ya Bukombe Ananias Alphone alisema kuwa wakulima wengi wameonyesha kuitikia naamini kuwa msimu ujao wataongezeka zaidi.


“Wakulima wengi wakipewa elimu wanafuata lakini hawana mbegu za kutosha jambo ambalo linapelekea waendelee kutumia mbegu ya asili ambazo zimekuwa zikishambuliwa na magonjwa ambapo tumeona tofauti kubwa na mbegu bora ambazo hazishambuliwi na magonjwa na pia zinastahili ukame”



Kwa upande wake Mtafiti wa zao la Karanga kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele Juma Mfaume alisema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa na kituo hicho ili kuweza kutoa elimu kwa wakulima wengi wa zao hilo waweze kuongeza uzalishaji.


 “Tumetoa mbegu kwaajili ya majaribio ambapo zimeenda kwa wakulima wa vijiji mbalimbali nchini ikiwemo kijiji cha Ryambamgongo ambapo tunafanya tafiti shirikishi katika mikoa hiyo ili kubaini ipi mbegu bora itakayowafaa wakulima  wa zao la karanga ndani ya Wilaya hiyo” alisema Mfaume

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI