Na Amon Mtega,Mbinga.
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameipongeza miradi inayofanywa na Halmashauri ya Mbinga mji Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma baada ya Mwenge huo kuridhia miradi saba ya Halmashauri hiyo.
Kaim akizungumza kwenye miradi hiyo ya aina tofauti amesema miradi ni mizuri ambayo imefuata taribu zote huku akitaka miradi ambayo imeshikwa na wakandarasi na ipo kwenye matazamio iweze kuangalia vema ili izidi kiwa bora zaidi.
Kiongozi huyo amesema kuwa Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitoa fedha nyingi miradi mbalimbali hivyo ni jukumu la Halmashauri kuzisimamia hizo fedha ili ziweze kuleta tija kwa Wananchi kwa kuwawekea miradi mbalimbali.
Aidha akiwa kwenye mradi wa ufyatuaji wa tofali za saruji kwenye kikundi cha Vijana kilichopo Muhekela kata ya Kilimani ameipongeza Halmashauri kwa kuwapatia mkopo wa zaidi ya sh.Milioni 20 kwenye kikundi cha Vijana hao ambacho tayari kinafanya kazi ya kufyatua tofali hizo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ndani ya Jimbo hilo.
Mbunge Mbunda akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Joseph Mdaka licha ya kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Mbinga Mji inayoongozwa na mkurugenzi Grance Quintine kwa kusimamia miradi hiyo.
0 Comments