Header Ads Widget

SHEKHE KIBURWA ATAKA WATOTO WALINDWE DHIDI YA USHOGA

 

Shekhe wa mkoa Kigoma Hassan Kiburwa (kushoto) akitoa hotuba kwenye sala ya Eid El Fitri iliyofanyika kimkoa kwenye msikiti wa Ijumaa Nyarubanda Halmashauri ya wilaya Kigoma

Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye kwenye sala ya Eid El Fitr iliyofanyika kijiji cha Nyarubanda


Na Fadhili Abdallah, Kigoma

SHEKHE wa mkoa Kigoma amewaongoza waislam mkoani humo katika ibada ya sala ya Eid El Fitri na kusisitiza kuwa wazazi wanapaswa kusimama imara dhidi ya malezi ya watoto wao ili wasiangukie katika mambo yasiyofaa  ikiwemo kuingia kwenye janga la ushoga na mapenzi ya jinsia moja.


Katika sala ya Eid El Fetri ambayo kimkoa ilifanyika kwenye Msikiti wa wa Ijumaa Nyarubanda Halmashauri ya wilaya Kigoma alisema kuwa kuharibika kwa jamii na kuingia kwenye mambo ya hovyo kunaanza na malezi mabaya yanatolewa na wazazi kwa watoto wao hasa kushindwa kusimamia misingi na mafundisho ya dini.



Shekhe huyo  wa mkoa Kigoma alisema kuwa ni lazima jamii iungane katika kukemea, kulaani na kupiga kelele za hapana kuhusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na ushoga ambavyo kwa siku za karibuni zimeonekana kushika kasi nchini huku vitendo hivyo vikielekezwa kufundishwa kwa watoto wadogo.

 

Sambamba na hilo Shekhe huyo wa mkoa Kigoma amewataka waislam kutumia kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama chuo kwa kuishi kwa mambo na vitendo walivyokuwa wanafanya kwenye mwezi huo ya kumcha Mungu na kutenda mema huku akikemea vitendo vya viongozi wa dini kuzusha taharuki na vurugu kwenye misikiti kwa kugombea uongozi.



Alisema kuwa katka baadhi ya maeneo mkoani humo kumekuwa na vurugu kwenye misikiti huku masuala ya kisiasa yakiwa sehemu za vurugu hizo kwa baadhi ya wagombea au viongozi waliopo madarakani kutaka kusimika watu wao kwenye misikiti huku taratibu za kupata uongozi kwenye misikiti zikivurugwa.

 


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye amewata waumini wa kiislam waishi kwa amani na upendo na kushirikiana kama ambavyo mwezi mtukufu wa Ramadhani umewaweka waislam kuwa watu wenye walioishi kwa amani na upendo.

 

Katika Salam za Eid El Fitr zilizotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Salum Kali alisema kuwa inawezekana kuishi kwenye dunia yenye amani na upendo ambayo hailazimishi silaha kubwa kubwa kutumika kulinda amani kwamba Mwezi wa Ramadhani umeonyesha kuwa wa tofauti na heshima kubwa kwa waumini wa dini ya kiislam.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliunga mkono kauli za kulaani na kukemea ndoa za jinsia moja na vitendo vya ushoga kwani alibainisha kuwa vitabu vyote vya dini vinapinga vitendo hivyo kwani hata umati wa kaumu Lutu licha ya kuwa na makasiriko na mchukizo maengo kwa Mungu haikuwa na vitendo hivyo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI