Header Ads Widget

MBARONI KWA KUTAKA KUMNAJISI BINTIYE



NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Mwanaume mmoja ajulikanaye kwa jina la Godbless Mushi mwenye umri wa miaka (39) Mkazi wa shibula Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kutaka kumnajisi Mtoto wake wa kumzaa.

Jeshi la polisi Mkoani hapa likitoa taarifa limeeleza kuwa mtuhumiwa alijaribu kufanya kosa hilo mnamo majira ya saa 04:00 usiku kwa mtoto wake mwenye umri wa miaka (5) ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa amelala katika chumba cha wazazi wake wakati mama ake akiwa anaendelea na shughuli za nyumbani ndipo mwanaume huyo alipata nafasi ya kujaribu kutaka kumfanyia kitendo Cha udhalilishaji wa kingono.

Mnamo tarehe 03.04 mwaka huu tukio hilo la kikatili liliripotiwa katika kituo Cha polisi kirumba na askari wa dawati la jinsia walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anaendelea kufanyiwa mahojiano zidi ya uuzalilishaji aliokuwa akitaka kumfanyia Mtoto wake wa kumzaa.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na mashahidi pamoja kumfanyia uchunguzi wa kitaalamu kupitia jeshi la polisi kitengo Cha dawati la jinsia na watoto Kwa kushirikiana na ustawi wa jamii na upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi linatoa  wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa na kutofumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na watu wengine vinavyofanyika majumbani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI