NA WILLIUM PAUL.
MBUNGE wa Jimbo la Same mashariki mkoani Kilimanjaro, Anne Kilango Malecela amesema kuwa hakuna aliyetajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali kuchezea hela za Watanzania atakayepona.
Anne Kilango ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuwa na uvumilivu wakati kipindi hiki wabunge wanapoisubiria ripoti hiyo ifike Bungeni.
"Rais Dkt Samia Suluhu Hasani, Wabunge na Watanzania tumechukizwa na taarifa ya CAG, Watanzania wamekuwa wakihisi sisi wabunge mbona hatuongei au tunefurahushwa nayo nikwambie tu tutaifanyia kazi ripoti hiyo kwa kuzingatia Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 143 mabano 4 pindi ikifika kwetu mtaona" alisema Anne Kilango.
Mbunge huyo alisema kuwa, Rais Dkt Samia Suluhu Hasani amekuwa akiangaika kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania hivyo hawezi kukubali kuona fedha zikichezewa hovyo.
Alitumia pia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuwa na uvumilivu kwani Wabunge ambao ndio wasemaji wao wanafuata taratibu kuhusu ripoti hiyo na kuwahakikishia kuwa hakuna yeyote aliyetajwa katika ripoti hiyo atakayepona.
"Rais na sisi Wabunge hatutakubali kuona yeyote aliyechezea hela za Watanzania akiendelea kuzunguka nchini tutahakikisha wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria" alisema Mbunge huyo.
Mwisho.
0 Comments