Header Ads Widget

MATUMIZI YA VANILA KUCHOCHEA MTU KUWA NA AKILI NYINGI.

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MKURUGENZI Mkuu wa Vanilla International Limited Simon Mnkondya ameitaka jamii kutumia zao la Vanilla katika matumizi ya Kila siku kwani zao hilo huchochea kuwa na akili zilizopitiliza Kwa binadamu.


Mnkondya amebainisha hayo April 4,2023 jijini Dodoma kwenye kikao Cha wadau wa zao la Vanilla.


Amebainisha kuwa ili kuweza kuwa na akili nyingi,hata wanasayansi na wanamuziki wakubwa duniani wamekuwa wakitumia malighafi inayopatika katika zao la Vanilla hali inayopelekea kuwa wabunifu na kubuni vitu mbalimbali vikibwa na vyakipekee.


Pia amebainisha kuwa kilimo Cha Vanilla soko lake linapatikana Kwa wingi katika nchi za uarabuni na Vanilla inayonuniliwa sana ni Vanilla ya gradi la kwanza.


Aidha katika kuuza zao la Vanilla kwa Duniani ya sasa Mnkondya amebainisha kuwa haina haja ya kubeba mzigo kupeleka katika nchi unaweza kuuza kupitia mtandao Kwa kuandika vigezo vya zao lako la Vanilla na wateja wakakufata wenyewe.


"Niwaeleze wakulima kuwa zao la Vanilla halitakiwi kulimwa kiholela na badala yake anawashauri wakulima kulima kilima cha pamoja yani (kilimo Cha Block Farming)," Amesema Mkurugenzi huyo.


Katika hatua nyingine ametahadharisha kuwa watu wanaolima zao la Vanilla wapo katika hatari ya kujiruhiwa kwani zao hilo lina bei sana na kupelekea kupata fedha nyingi.


Hata hivyo akiongelea kuhusu vyama vya ushirika Mnkondya amebainisha kuwa vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaibia wakulima bila kuwatengenezea masoko ya uhakika na badala yake vimekuwa vikitengeneza wezi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI