Header Ads Widget

MALINYI WAZINDUA CHANJO KWA WATOTO

 



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mheshimiwa Pius Mwelase amezungumzia umuhimu wa chanjo kwa vizazi vya Sasa ambapo amewataka wazazi kujitokeza kuwapatia chanjo watoto ili kuweza kujikinga na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri afya za watoto



Kauli hiyo ameitoa wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo Wilayani Malinyi lililofanyika April 25 mwaka 2023 ambapo litaendelea mpaka April 29.


"Niwaombe wazazi kujitokeza kuwapa chanjo watoto wetu ambao wanalengwa kupata chanjo hizi kwa ajili ya kulinda afya zao"alisema.



Kwa upande wake mratibu wa chanjo Wilayani Malinyi Eliesekie Mbwambo amesema zoezi hilo litalenga watoto wote ambao wanahitaji chanjo na litafanyika wilaya nzima ya Malinyi.


"Naungana na Mheshimiwa mwenyekiti kutoa wito kwa wazazi kujitokeza kuwapa chanjo watoto zinasaidia kuondoa magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kukingwa na chanjo hizi"alisema.



Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Muungano Waryuba ndiye amezindua zoezi hilo la chanjo na kuanza kutoa kwa watoto wote wanaolengwa kupatiwa chanjo Bure.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI H/W MALINYI.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI