Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angela Mabula amesema hayuko tayari kuona madudu yanayoendelea katika Jiji la Dodoma yakiendelea katika utawala wake kutokana na vitendo vya ubadhilifu vinavyoendelea katika Sekta ardhi katika Jiji la Dodoma.
Aidha amepiga marufuku kwa watendaji wa waadilifu wanaopima viwanja katika eneo la makabuli na sehemu ya kingo za mto ili kugawia wananchi maeneo hatarishi akitaja tabia hiyo kama tamaa isiyofaa.
Aidha Waziri ameonya kuwa kuna baadhi ya Watendaji wana tabia ya ucheleweshaji au kutoa namba wa malipo(control number) kwa rushwa na kuonya kwanini mwananchi anunue haki yake jambo ambalo ni kinyume na maadili.
Waziri Mabula amebainisha hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi kilichowakutanisha Watendaji Sekta ya Ardhi pamoja na makampuni ya Upimaji katika Mkoa wa Dodoma leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Mhe.Mabula amewataika vijana wote wanaojitolea katika jiji la Dodoma kuacha kazi hiyo mala moja kwani wamekuwa wakifanya vitendo vya ukiukwaji wa maadili katika Sekta ya ardhi.
‘’Vijana hawa wamekuwa wakimiliki magari pamoja na majumba makubwa je vijana hawa wanajikimu kwa kutumia nini kwani hawana mishahara lakini wanaendelea na kazi bila hajila.
Waziri Mabula akaoji ni wapi Vijana hawa wanapata fedha nyingi bila kula rushwa kwani wameombwa kusaidia kazi katika miradi ya Wizara inayoendelea na kuikataa kazi hiyo kwani hwako tayari kufanya kazi ya ujila huo.
Kufuatia hali hiyo Waziri Mabula akaagiza Mkurugunzi wa Jiji la Dodoma kuondoa vijana hao wenaojitolea katika sekta ya ardhi kwani wao ndio wanaleta sintofahamu ya Migogoro katika Sekta ya Ardhi.
0 Comments