Header Ads Widget

"AZAM FC" YAJITOSA KULINDA MAADILI.




Timu ya soka ya Azama FC imejitangaza  rasmi  kuwa Balozi wa ajenda ya kuhamasisha maadili mema na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwa watoto ndani ya jamii.


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC Abdulkarimu Amin maarufu 'Popat' amewambia Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuwa, klabu hiyo itatumia Majukwaa yake kulinda, kutangaza na kuhamasisha Maadili Mema ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali kupinga vitendo vya ukatili nchini.


"Tukiwa familia ya  mpira tunaunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwani jambo la ukatili linagusa kila mtanzania, natoa rai kwa klabu zingine za Michezo kuungana kupinga ukatili na kuhimiza maadili mema" amesema Popat.



Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,  Dkt. Dorothy Gwajima ameishukuru na  kuipongeza klabu hiyo kwa kukubali kuwa sehemu ya Mabalozi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na kwa Watoto na kusema ni jambo la kuigwa na muhimu kwa manufaa ya Jamii.


"Tumebaini nguvu kubwa ipo kwenye Michezo, hivyo kuibeba ajenda ya kuhimiza Maadili na kuipeleka kwenye jamii ni muhimu, ifahamike faida za Michezo mojawapo iwe ni kuwaunganisha watu kupinga vitendo viovu" amesema Waziri Gwajima.


Azam FC inakuwa Klabu ya Pili hapa nchini, kuunga mkono jitihada hizi za Serikali, kwani mapema Mwezi Machi, 2023 Klabu ya Yanga yenye makazi yake eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam ilitangaza azma hiyo ya ajenda yakulinda maadili.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI