Na Titus Mwombeki, Matukio Daima App Kagera.
WANAOHISIWA kuwa na dalili za Ugonjwa Marburg Mkoani Kagera Wamefikia 205 Kutoka 193 kama ilivyokuwa imeelezwa na mganga mkuu wa Serikali Prof.Tumain Nagu Machi 23 Mwaka huu Akiwa Mkoani Kagera.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa uliopo Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kuwa mpaka sasa hakuna visa vipya vya wagonjwa wala kifo chochote kilichotokea kuwa na ugonjwa huo nje na awale walioripotiwa hapo awali.
"Bado tuna visa nane ikiwa ni vifo vitano na wa tatu bado wanaendelea na mabibabu, lakini washukiwa wa waliochangama na wagonjwa huu wameongezeka na kufikia 205 ambao ni wanafamilia na wataalamu wetu wa afya ambao wali hudumia wagonjwa hao, hii ni dhahili kuwa ugonjwa huu haujatoka nje ya familia ambazo zimeathiliwa na ugonjwa huo"
Aidha, watu hao waliotengwa sio wagonjwa bali na hawana dalili zozote ila wamezuiliwa kwa muda ili kuwalinda wenyewe endapo watapata dalili pamoja na kuilinda jamii huku akisisitiza kuwa mtu kama hana dalili za ugonjwa huo hawezi kumuambukiza mtu mgonjwa mwingine.
"Ugonjwa wa Marburg. uambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mtu mwingine analogical maji maji wa mgojwa mwenye ugonjwa huo, mate, mkoja, damu au kinyesi kutoka kwa mtu aliyefariki kwa ugonjwa huo au mtu anayeonyesha dalili za ugonjwa wa Marburg, vilevile ugonjwa unaweza kutokea kutoka kwa wanyama kama vile popo, nyani na nyani kwenda kwa binadamu endapo atakula au kugusa mizoga ya wanyama hao" amesema waziri Mwalimu.
Aidha amesema kuwa timu ya wataalamu wabobezi wa kupambana na ugonjwa huo wameishawasili mkoani Kagera ili kusaidizana na wataalamu wengine wa afya walioko mkoani humo huku amewataka wananchi mkoani Kagera kuendelea kuchukua taadhari za kujikinga na ugonjwa huo kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono.
Sambambana hilo amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa afya inaendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kuanza kupima joto la wasafiri wote wanaoingia na kutoka ya nje ya mkoa wa Kagera huku akiwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato.
0 Comments