Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MFUKO wa Mawasiliano kwa wote UCSAF umetoa msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya jumla ya Shilingi Milioni 8350000 katika kituo cha kulelea Watoto wenye mahitaji Maalum cha Tumaini Foundation kilichopo Ihumwa Dodoma huku wito ilitolewa kwa jamii kuwa na utaratibu wa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji Maalum.
Akiongea kabla ya kukabidhi msaada huo Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema ikiwa bado ni mwezi wa wanawake duniani wameona ni vyema wanawake kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kurudisha kidogo wanachopata kwa kuwakumbuka Watoto wenye uhitaji .
Aidha amesema kila mwaka mwezi Machi kwenye sherehe za wanawake duniani wamekuwa wakifanya hivyo kwa kutoka na kuwatembea watu wenye uhitaji kwao ni upendo uliotukuka
"Hapa naomba kukumbusha Jambo kwa jamii kuelewa kuwa Mtoto wako wa leo ni yatima ya kesho hivyo hata huko nyumbani tuwalee kwa misingi hiyo bila kusahau kuawajengea upendo kupenda na kuwathamaini wengine, "Amesema Mtendaji huyo Justina
Awali akiwakaribisha katika kituo hiko Mkurugenzi wa Tumaini Foundation Tumaini Mvuyo amewashukuru wanawake wa UCSAF kwa kuguswa kwao na kupeleka msaada kwa Watoto wanaolelewa na kituo hicho cha Tumaini
Mkurugenzi huyo amesema kituo cha Tumaini kinahudumia jumla ya Watoto 350 nchi nzima huku Watoto 100 wakiwa katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda.
Amesema kituo hicho cha Tumaini Kimekuwa kikiwaibua Watoto wenye Changamoto mbalimbali Kama wenye ulemavu,wanaoishi na virusi vya ukimwi na yatima wale wote waliopo pembezoni walifichwa ndani .
"Tunashukuru tunawatoto wengi ambao tumewaibua baada ya kufichwa ndani na ndugu zao wa karibu kwa muda mrefu lakini leo hii tupo nao hapa na wameweza kusimama wenye," Amesema Mkurugenzi Tumaini
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameomba jamii kuendelea kujitolea kwa kuwakumbuka Watoto wenye uhitaji ambapo ameeleza kituo chicho hakina wafadhili bali Kimekuwa kikiendeshwa Fedha zao Kama wana kituo na misaada ya watanzania .
Naye Suzan Zakayo Mtoto anayelelewa katika kituo cha Tumaini Ihumwa ameshukuru taasisi hiyo ya serikali ya UCSAF kwa kuwaletea na kuwapatia msaada huku akisema wamefanya Jambo jema na Mungu atawabariki na kuwaongea pale walipotoa.
0 Comments