Header Ads Widget

WAKULIMA WA UFUTA KISARAWE WAOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAAFISA UGANI

 


Na mwandishi wetu, Pwani


Wakulima wa Zao la Ufuta Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani wameiomba serikali kuwaongezea maafisa ugani ili waweze kupata huduma kwa ukaribu baada ya kuhamasika kulima zao hilo.


Akizungumza mkulima wa ufuta kutoka kijiji cha  kihare Salum Kombwe  alisema kuwa wamehamasika kulima zao hilo japo hawana utaalamu hivyo kuomba serikali kuwaongezea maafisa ugani na pia kuiomba tari kuongeza mafunzo kwa ili kulima kilimo cheneye tija.


Aidha amesema zao hilo lina faida nyingi kiuchumi na kiafya hivyo mafunzo hayo yataongeza hali na hamasa kwa wakulima na wasio wakulima kutamani kulima ufuta katika wilaya ya hiyo ya kisarawe.


kwa sasa tunamtumia afisa kilimo wa kata ya jirani baada ya afisa kilimo wa kata wetu kwenda masomojni hata hizi mbegu tulipewa tukapanda bila kupata maelekezo yoyote jambo ambalo linafifiisha jitihada za tari za kuongeza uzalishaji wa ufuta nchini.



Hatuna vitendea kazi ni changamoto kwetu hususani trekta lakini pia tukipewa malambo makubwa tunaweza kupata maji kwa wakati  na tukalima zaidi ingawa wanaotukwamisha ni wafugaji wanatupa wakati mgumu kwakuwa mifugo yao inatuathiri”


Nae Omary Diviele mkulima kutoka kijiji cha kihare wilayani kisarawe anasema kuwa elimu kubwa itolewe ili kuongeza uhamasishaji kwakuwa zao hilo ni geni na linawapa wakati mgumu.


“Tunaomba tuongezewe wataalam wao unatuathiri wakulima  lakini pia tuonaomba akipatikana mtaalam wa ufuta aje huku atuokoe tulime ufuta zaidi”



Mratibu wa Program ya zao la Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda anasema kuwa amefika katika shamba la pamoja wilayani Kisarawe Wilaya ya Kihale heka 400.


“Wanahitaji elimu ya matumizi  sahihi ya namna ya upandaji  namna ya kupanda elimu inahitajika hasa nafasi matumizi ya teknologia ya kilimo udhibiti wa wadudu mimea jinsi ya kutumia mbolea”


“Tumewafikia kwakuwa tuko tayari kutoa ushirikiano kwa ili kuweza kukalisha ndio maana tumeweka mashamba darasa ili kuweza kuongeza uzalishaji wa zao hilo nchini”



Nae Ofisa kilimo msaidizi kutoka Tari Naliendele Nicko Lukoya anasema kuwa wakulima wawasikilize  na kufuata maelekezo ya wataalamu ili waweze kulima kilimo bora chenye tija kwao.


“tunaona shamba wamelima vizuri wamepalilia na kuweka dawa za kudhibti wadudu tunawashauri waendelee kutumia mbolea za maji na dawa za kuua wadudu ili kuwadhibiti”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI