JUMLA ya shilingi bilioni 1,409,332,000(bilioni 1.4)zimetolewa na serikali Wilayani Malinyi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Miradi hiyo ni ukarabati wa barabara na matengenezo ya sehemu korofi ,kuimarisha sehemu korofi na ujenzi wa makalavati katika barabara zinazosimamiwa na Wakala wa usimamizi wa barabara za vijijini na mjiniTARURA wilaya ya Malinyi.
Meneja wa TARURA wilaya ya Malinyi Mhandisi Charles Mang’era amesema fedha hizo zinahudumia miradi nane katika wilaya hiyo.
Amefafanua kuwa kati ya miradi nane miradi minne imefikia asilimia 70,miwili asilimia 50 na miwili ikiwa asilimia 40.
Ameitaja miradi ambayo inatekelezwa kupitia fedha ya bajeti ni mradi wa ukarabati wa barabara Itete Njiwa kwa kiwango cha changarawe kilomita 5 wenye thamani ya shilingi milioni 290,680,000,mradi wa ukarabati wa barabara ya Tanga kwenda Biro kilomita 6.5 wenye thamani ya shilingi milioni 299,492,000.
Miradi mingine ni ule wa ukarabati wa barabara ya Ngoheranga kwenda Kikove wenye kilomita 5 kwa shilingi milioni 465,900,000,matengenezo ya maeneo korofi vijiji vya Salamiti,Kiswago,Mtimbira,Msalaka,Itete Sekondari,IteteNjiwa na Ipera asilia huku yakifanyika matengezo ya muda maalum ya barabara za Mkalimoto,Kalengakero,Usangule,Likeya,Mafinji,Madabadaba,Kiswago,Salamiti,Mtimbira,Msalaka,Itete,Minazini,Itumbika,Sofimajiji na mtimbira ambapo maeneo yote hayo yanatumia kiasi cha shilingi milioni 282,486,500.
Miradi mingine ni ule wa kuimarisha sehemu korofi ambao upo katika vijiji vinavyounda Tarafa za Ngoheranga,Mtimbira na Malinyi una thamani ya shilingi milioni 242,570,000 ambapo umepitia maeneo ya Lugala,Misegese,Ngoheranga,Kikove,Malinyi ,Igawa,Tanga,Ihowanja,Miwangani na maeneo korofi ya barabara maalum ya Mtimbita JCT,sokoni,Igawa,Bomani sekondari,Kipingo,Lugala,Ngoheranga na Ihowanja.
Katika miradi inayotekelezwa na TARURA pia upo mradi wa ujenzi wa makalavati baraba za Mtimbira,Itete,Sokoni,Itete,Minazini,Itumbika,sofi majiji na mnadani ambapo mradi huu unatekelezwa kwa kiasi cha shilingi milioni 68,306,000.
Mhandisi Mang’era amesema mradi mwingine ambao unatekelezwa ni ule wa matengenezo ya kawaida karika barabara za Malinyi,Igawa,Kipingo,Lugala,Misegese,Tanga na Biro ambao unatekelezwa kwa kiasi cha shilingi milioni 53,190,800,000.
Katika utekelezaji wa bajeti hiyo yam waka 2022/2023 serikali kupitia TARURA pia inatengeneza barabara za Mtimbira kwa kiwango cha changarawe.
Amezitaja changamoto ambazo zinaikabili miradi hiyo kuwa ni pamoja na makundi ya mifugo kuingilia ujenzi wa miundombinu ya barabara ambazo husababisha mmomonyoko katika baraba za kiwango cha changarawe na udongo pamoja na shughuli za kibinadamu kama kilimo ambazo hufanywa kandokando ya barabara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-H/W MALINYI.
0 Comments